"Natumaini ataelewa kwanini alikuwa yupo vizuri!!" Mourinho amempa changamoto Pogba kuingoza Manchester United kwenye mafanikio kama alivofanya kwa Ufaransa. - BZONE

"Natumaini ataelewa kwanini alikuwa yupo vizuri!!" Mourinho amempa changamoto Pogba kuingoza Manchester United kwenye mafanikio kama alivofanya kwa Ufaransa.

Share This
Jose  Mourinho amempa changamoto Paul Pogba baada ya kuingoza Ufaransa kubeba kombe la Dunia na sasa amemgeukia kwa upande wa klabu yake na anataka afanye kama alivoweza kufanya kwa Ufaransa ili waweze kulibeba taji la Ligi kuu.

Image result for paul pogba

Pogba ameonesha pale alipokuwa Les Bleus Urusi kwamba yeye ni ufunguo tosha kwa Didier Deschamps aliweza kushinda goli la tatu kwenye ushindi wa 4-2 kwenye fainali dhidi ya Croatia na Mourinho akegeukia upande wa pili baada ya kuona kiwango chake hicho.

"Kushinda kombe la Dunia inaweza ikawa ni kitu chanya kabisa, ni ngumu sana kusema kushinda kombe la Dunia sio nzuri kwa safari ya mchezaji yeyote ni kitu cha kufurahisha na ni kizuri sana."

Image result for paul pogba

"Wachezaji wazuri wengi na hawajawahi kupata kuwa ata mabingwa Dunia au mataifa yao hayajawahi kubeba taji la Dunia au mataifa yao hayana nguvu ya kutosha."

Image result for jose mourinho and paul pogba

"Kwa Paul nafikili ni kombe lake la kwanza la Dunia kulibeba na timu yao ni timu ya vijana karibuni kikosi kizima ukiachialia mbali goli kipa Hugo Lloris kwahiyo mimi nahisi maisha yake kwenye kikosi cha Ufaransa ni marefu sana." Alisema Mourinho.

No comments:

Post a Comment

Pages