Naona kama kumeanza Kunoga..! Wenyeji wawashtua mabingwa wa 2010 kwa mikwaju ya penati ndani ya Moscow. - BZONE

Naona kama kumeanza Kunoga..! Wenyeji wawashtua mabingwa wa 2010 kwa mikwaju ya penati ndani ya Moscow.

Share This
Uhispani walijikuta wanalazimishwa mikwaju ya penati na Urusi huku wakijikuta wanatupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 kwenye atua ya 16 bora.

Pande zote mbili ziliweza kujipatia magoli kwenye vipindi viwili tofauti  huku Sergei Ignashevich akijifunga yeye mwenyewe kabla ya Artem Dzyuba kusawazisha makosa hayo kwa mkwaju wa penati, Uhispani walianza vizuri wakimiliki mpira kwa asilimia kubwa sana kwenye mchezo.Pale goli la uongozi lilipo patikana kwa Juhudi za Sergio Ramos tulijua kuwa wenyeji washapotea wenyeji washapotea na walikuwa na kazi kubwa sana ya kusawazisha goli ilo lakini mimi binafsi nilikuwa nina imani nao.Ila mimi naweza nikasema kuwa Uhispania wamejitakia wenyewe ili janga kwasababu Andres Iniesta aliachwa nje kwenye kikosi kilichoweza kuanza huku akiingia dakika ya 25 kwenye kipindi cha pili huku Iago Aspas akichukua nafasi ya Diego Costa ambae siku ya leo akuweza kutema cheche zake.Ila pongezi nyingi ziende kwa kipa wa Urusi ambae ameonesha umuhimu wake wa kuwa Nahodha na kipa wa kuaminiwa kwenye kikosi hiki cha wenyeji ambae baada ya dakiak 120 ndio aliinuka kuwa shujaa wa Urusi kwa siku hii ya leo.

No comments:

Post a Comment

Pages