Lakini Madrid wanaonekana wameweka vyema ngome zao za kuweza kumnasa kinda huyu kwa dili la Pauni Milioni 40 kwajili ya kumdondosha Mbrazili huyu Bernabeu.

Kupitia Gazeti la Marca limesema kwamba mabingwa hawa wa Ulaya teyari wameshapiga pini vikwazo vyote vya Barcelona na kufanya mambo yote kuwa poa kwenye kufanya biashara hiyo na uongozi wa Santos.
:strip_icc()/s.glbimg.com/es/ge/f/original/2018/06/07/28759169148_dc66c3c648_o.jpg)
Na inaelezwa kwamba mshambuliaji huyu ameweza kufanya vyema msimu uliopita na amepewa uhakika wa kuweza kujiunga na Real Madrid na kama Madrid wakifanikiwa kufanya biashara hii watakuwa wameokota Embe Dodo kwenye Mnazi na kuwaumiza kichwa wapinzani wao.

Barcelona wameweza kuweka nguvu zao nyingi kwajili ya kumpata Rodrygo ambae ameshinda magoli matano kwenye michezo kumi na moja ya Santos.

No comments:
Post a Comment