
Mshambuliaji huyu wa Manchester City ameweza kurudi Uingereza kwenye kikosi chake baada ya Joachim Low kumuacha kwenye kikosi chake kinachoenda Urusi na tabia ya Sane sidhani kama ndio kikwazo kikubwa cha yeye kuachwa kwenye kikosi cha ujerumani.

Mshambuliaji huyu mwenye miaka 22 japo akucheza kwenye kiwango kinachotakiwa Siku ile ya Jumamosi dhidi ya Austria lakini bado ilikuwa ni shtuko kubwa sana kwa Wadau wake.

Hii imekuja kuwashtuko baada ya kuwa mchezaji tegemezi kwenye kikosi cha City alichoweza kukisaidia kubeba taji la Ligi na yeye binafsi kujibebea tuzo ya PFA yakuwa mchezaji bora chipukizi.

Sasa tunamuona anatumia mapumziko akiwa nje ya mashindano makubwa huku bado akiwa anaendelea kujipanga kwajili ya kufungua mazungumzo na Manchester City juu ya mkataba wake mpya ambapo ilikuwa imepangwa baada ya Kombe la Dunia.

No comments:
Post a Comment