
Goli la Hirving Lozano kwenye kipindi cha kwanza lilikuwa linatosha kuwapa Mexico alama tatu muhimu ambao kwasasa wamejiwekea nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye kundi lao.
Timo Werner aliweza kupata nafasi iliyo safi kwenye kipindi cha pili vijana wa Joachim Loew ni lazima wajiweke sawa kwenye mchezo dhidi Sweden na Korea Kusini ili waweze kuendelea kwenye hatua ya 16 bora.

Ikumbukwe Manchester United walikuwa ni moja ya klabu ambazo zinamuwinda Hirving Lozano huku Mexico walikuwa tishio kubwa sana kwenye goli la Ujerumani

Ulikuwa mchana mbaya sana kwa Joshua Kimmich akichukua majukumu ya winga kutokea kulia nyuma lakini alijikuta majukumu yakiwa mazito sana kwake yeye na kukosa balance ya kuweza kumuhandle Hirving Lozano, mchezaji huyu wa Bayern Munich inasemekana ni moja kati ya wachezaji wazuri makinda wa kijerumani.

Moja kwa Moja atuwezi kulaumu kukosekana kwa Leroy Sane lakini kama angekuwepo ninaamini angefanya utofauti wowote kwenye mchezo huu wa leo wejaribu kuangalia alivoweza kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya Uingereza na klabu yake ya Manchester city na kunyakua tuzo ya PFA ya kuwa mchezaji bora wa mwaka kinda.
Ninajua hii imewachanganya wajerumani wote ambao hawakutarajia kabisa haya matokeo ya mchezo wa Ufunguzi lakini kama wakifanya vyema michezo miwili ijayo wanaweza wakasonga mbele.

No comments:
Post a Comment