Nilikuwa nasikiaga yajayo yanafurahisha sikuwa naelewa ila sasa naanza kuelewa..! Nilianza kuifatilia Safari yake Tangia alipokuwa Friends Rangers ila sasa kuna kitu nimejifunza kutoka kwake. - BZONE

Nilikuwa nasikiaga yajayo yanafurahisha sikuwa naelewa ila sasa naanza kuelewa..! Nilianza kuifatilia Safari yake Tangia alipokuwa Friends Rangers ila sasa kuna kitu nimejifunza kutoka kwake.

Share This

Ndoto ndoto..! Kwenye Maisha tuliokuwepo hapa Duniani nina amini kila mmoja ana ndoto za kuwa mtu fulani kwenye hii sayari tulio kuwepo ila sasa kuna wale ambao wanaini juu ya ndoto na vipawa walivyojaliwa ila kuna wale wasio amini juu ya hii.


Huyu jamaa ni rafiki yangu wa kweli sana na pale nilipomjua tuu nkaanza kumfatilia na kuona atafikia wapi maana jamaa alikuwa anaamini kwa kile anachokifanya ata kama asipo pata leo wala kesho.Eleuter Mpepo ni kijana ambaye ametokea katika jiji maarufu Tanzania kwa ukijani wake wajanja wenyewe wanapaita ‘The Grern City’ safari yake ya soka rasmi ilianzia pale alipo pata nafasi kwenye  kikosi cha Azam B aliwatumikia wana lamba lamba hawa kwa mda wa mwaka mmoja baada ya hapo ndipo akajachukulia na vijana wa Rangers ambao unaambiwa ndio wenye Kinondoni yao.

Ila niamini nachokwambia kwa nafasi yake anayocheza uwanjani kama huna matumaini ya kufikia ndoto utakuja jikuta ufikii chochote na ndoto zako za kuchezea klabu kubwa na ligi kubwa zimaishia hapo hapo ila ni uvumilivu, Juhudi na kumuomba Mungu kila siku ndio silaha pekee Mpepo aliyokuwa nayo mfukoni na ndio iliomfanya mpaka kufika pale alipo sasa.

Image may contain: 1 person, playing a sport and outdoor

Mimi nazani maafande au wanajela jela hawakukosea kumpa mikoba ya mashambulizi pale walipomuonaga kwenye jiji ilo la mbeya kwenye moja ya timu iliyokuwa inashitiki ligi Daraja la kwanza na Mpepo hakuiacha fursa iende zake na akawaonesha kwamba hamkukosea kunipa mikoba ya mashambulizi na aliwaumiza baadhi ya vilabu kwenye ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita, sasa yupo Singida United ni klabu kubwa sana sasa Tanzania Bara ni klabu yenye ndoto ya kufika mbali na ndomana ata sishangai kuwachukua wachezaji kama Mpepo kwasababu nao pia wanandoto nadhani hapa unanielewa Vizuri.

Image may contain: 3 people, people standing, grass, outdoor and nature

Anyway najua utaona kama ni kitu rahisi sana ila ebhana eeh ukae ukijua kuna kitu cha kujifunza hapa na ndomana ukisikia yajayo yanafurahisha ujue hakuna alietarajia kama kitachokuja kitakuwaje ebu sikia najua una ndoto za kuwa mtu fulani iwe kwenye nyanja tofauti nachukua fursa hii kupitia mfano wa kijana huyu Mpepo laah laah..!  Usikate tamaa ta kama watakupinga watakucheka.

No comments:

Post a Comment

Pages