Ronaldo hakamatiki sasa Ebhana, Baada ya kuwapa adhabu Morocco ajiwekea rekodi nyingine barani Ulaya. - BZONE

Ronaldo hakamatiki sasa Ebhana, Baada ya kuwapa adhabu Morocco ajiwekea rekodi nyingine barani Ulaya.

Share This

Cristiano Ronaldo kwa sasa ndio mfungaji bora Ulaya kwenye historia ya ngazi za Kimataifa baada ya kufunga Goli lake la 85 kwa Ureno kwenye ushindi wao walio upata wa 1-0 dhidi ya Morocco.

Related image

Nyota huyu wa Real Madrid aliweza kufunga goli pekee siku ya leo ndani ya dakika nne baada ya mchezo kuanza wakimenyana na Morocco kwenye mji wa Moscow akifikisha magoli manne kwenye mashindano haya baada ya Hat trick yake ile ya kwanza dhidi ya Uhispania kwenye mchezo wa ufunguzi.

Related image

Na hiyo ndio iliompelekea kuweza kumpita gwiji wa Hungary Ferenc Puskas na kujiweka kwenye Orodha ya wafungaji bora mda wote kwenye ngazi ya kimataifa huku akiwa nyuma ya magoli 24 nyuma ya mkongwe wa Iran Ali Daei.

HII NDIO ORODHA YA WAFUNGAJI BORA MDA WOTE KWENYE NGAZI YA KIMATAIFA.

1. Ali Daei (Iran) - 109
2. Cristiano Ronaldo (Portugal) - 85
3. Ferenc Puskas (Hungary) - 84
4. Kunishige Kamamoto - (Japan) - 80
5. Godfrey Chitalu (Zambia) - 79

No comments:

Post a Comment

Pages