Sawa tunajua lazima ushikiliwe na utakiwi kuachwa tunajua unatakiwa kubebwa ila na wewe mwenyewe ujibebe ila kwasisi atuwezi kukuchoka kwasababu wewe ni ndugu yetu na tunajua fikra na uwezo wako unaposhika kalamu na karatasi laah..! Tunakujua vizuri unapokuwa nyuma ya M.I.C
Mimi bado nafikilia sana sijui nitafute dawa ya aina gani ya kukufanya urudi kwenye game na huache hiyo michezo unayofanya maana atuwezi kukuchunga kama mnyama.
Sikia Chid mwanangu ebu jaribu kuangalia pembeni yako kuanzia kulia, Kushoto, Mbele na nyuma jaribu kujiuliza tumeshawapoteza kwa kile walichokuwa wanakifanya au kukitumia ila jaribu kujiuliza ndugu yako Chillah na Dada yako Ray c waliweza vipi kuacha hiyo kitu na hizo drama.
Nakuachia na kukupa mda kidogo wa kujitathimini wapi unapoenda na nini unachokifanya na utaishia wapi japo wote tunajua ubaya wa hiyo kitu kwa leo ndugu yako sina mengi juu yako ila ukae ukijua nikiwa ni moja ya shabiki yako wa Damu na wengine tumechoka usikae kila mda unajipa moyo kwamba mashabiki zako tupo mda wote ata kama ukifanya ujinga sisi tunamtaka King Kong radi sauti ya chuma tunaemjua mda wote acha hiyo kitu na hayo mambo.

Game still bado ipo na still inakusubiria ushakuwa mkubwa wewe sasa usijifanye ujui ila sawa kwa kipindi kigumu ulichopitia ujui zuri wala baya kwasasa Come on Men naumia sana kukuona wewe vile.
No comments:
Post a Comment