Kwani Manchester United waliwazidi vipi wapinzani wao City kumnyakua Fred? - BZONE

Kwani Manchester United waliwazidi vipi wapinzani wao City kumnyakua Fred?

Share This
Manchester United wameweza kushinda shindano ambalo walilokuwa wakichuana na Kocha wa City Pep Guardiola kwenye kumnyemelea Mbrazil Fred.



United siku ya Jumanne waliatangaza kwamba wameshafikia makubaliano na kiungo wa Kibrazil mwenye umri wa miaka 25 pamoja na shakhtar Donetsk, Kiungo huyo anajianda kusaini mkataba wa miaka mitano kwajili ya kujisogeza OLD TRAFORD baada ya mashetani wekundu kushinda mbio za kumfukuzia kiungo huyo.

Image result for fred

City walikuwa wakuvutiwa sana kumdondosha Mbrazil huyo kwenye ardhi ya Etihad ambapo walianza kumfukuzia tokea mwezi Januari, mbali na hiyo imesemwa kwamba Majeruhi na Nahodha wa City Vincent Kompany alikuwa akimtamani Fred kutua City kulingana na gazeti la Metro.

Image result for fred

Kwasasa Fred yupo kwenye majukumu ya Taifa lake akiwa na timu yake ya Taifa yani Brazil kwenye kombe la Dunia huko Urusi huku kutangazwa rasmi na klabu yake mpya ikiwa bado Jose Mourinho anatakiwa kusubiria mpaka pale kombe la Dunia litakapo malizika ili kumpata nyota huyo.

Image result for fred

Rivaldo ni mtu wa karibu sana na Mourinho ambao washawahi kuwa wote Barcelona na anajua vizuri mbinu za Mournho aliweza kufunguka na kusema "Fred ni mchezaji mzuri sana kama walivo wengine pale unapompeleka kwenye taifa jingine atatakiwa apate mda kidogo wa kuzoea mazingira mapya."

No comments:

Post a Comment

Pages