Hii ni Habari mbaya kwa Bale? Hii inamaana gani kwa Real Madrid kufanya uteuzi wa kuahtukiza..kwa kumchagua Lopetegui..! - BZONE

Hii ni Habari mbaya kwa Bale? Hii inamaana gani kwa Real Madrid kufanya uteuzi wa kuahtukiza..kwa kumchagua Lopetegui..!

Share This
Real Madrid wamethibitisha kwamba Julen Lopetegui ndio atakuwa mrithi wa Zinedine Zidane siku ya Jumanne huku kibarua chake kikianza baada ya Kombe la Dunia akiwa amepewa ofa ya miaka mitatu.

Image result for Julen Lopetegui

Zidane aliachia ngazi baadya ya kushinda mara tatu mfululizo taji la klabu bingwa Ulaya akiacha viatu vikubwa sana kwenye dimba la Santiago Bernabeu, inaonekana hakuna alietaka kibarua hicho lakini Lopetegui amekinasa akikichukua kikosi icho msimu ujao..

Nimejaribu kuangalia uhamisho huu na unamaana gani kwenye klabu ya Real Madrid pamoja na wachezaji kama Gareth Bale.

Image result for Julen Lopetegui

Kwenye Dunia na utandawazi tuliokuwepo sasa hivi inaonekana kwamba vyombo vya habari na waandishi kama sisi tunaushawishi mkubwa sana kwenye mipango ya Klabu yoyote Duniani lakini Madrid wametupa ndoano kwa Lopetegui akitokea kusiko julikana.

Na kama Marca ambao wapo karibu na Raisi wa Madrid Florentino Perez hawakuwa na wazo lolote kama kocha huyu mpya angechaguliwa ikumbukwe kwamba Lopetegui alisaini mkataba mwengine na Taifa la Uhispania mpaka Euro ya 2020 na nimekaa nimejiuliza kuwa Chama cha soka Uhispania hawajaliona hili.

Image result for Julen Lopetegui

Akiteuliwa kwenye Neema ya Kombe la Dunia hii inaweza ikawa inawachanganya mabingwa wa Kombe hili mwaka 2010 kulibeba taji hilo tena, Focus itahamia kwa wachezaji kwenda kwa Kocha na hali ya hewa ya kwenye camp yao Urusi itakuwa imebaki kwenye viulizo vingi.

Ikumbukwe Lopetegui ambae kwenye msimu wa 2008-09 alishawahi kuifundisha Madrid lakini akiwa na kikosi B alikuwa kwenye Rada ya madrid kabla ya kuwa kocha wa Porto, Baada ya Ushindi wa 3-1 dhidi ya Bayern Munich kwenye klabu bingwa Ulaya hatua ya Robo fainali mwaka 2015 mishe mishe za kumnyemelea kocha huyo zilianza lakini washika nyundo wa Ujerumani waliwaumiza wapinzani wao kwa goli 6-1 kwenye mzunguko wa pili kila kitu kikaenda kuwa kimya.

Image result for Julen Lopetegui

Lopetegui ameshawahi kufanya kazi na kikosi cha Uhispania U19, U20 pamoja na U21 kwahiyo madrid watakuwa na matumaini anaweza akaleta mabadiliko kwa wachezaji wadogo ila Lopetegui ameshawahi kushinda Euro U19 mwaka 2012 pia akashinda Euro U21 mwaka uliofatia yani 2013

Kwasasa yupo na kikosi cha kwanza tangia alipochaguliwa mwaka 2016 na alwatoa wale wakongwe wote na kuwaweka vijana wenye vipaji venye njaa.

Image result for Julen Lopetegui

Kuchaguliwa kwa kocha huyu kunaweza ikawa taarifa njema kwa baadhi ya wachezaji lakini ikawa mbaya kwa wengine lakini faida kubwa ipo kwa Isco lakini Lopetegui anahusiano mzuri na wachezaji wadogo wa Kihispania ambao baadhi yaoa ameshawahi kufanya nao kazi kwenye vikosi alivyoweza kupitia.

Image result for gareth bale

Ila kwa ndugu yangu Gareth Bale anaweza asifurahi kabisa taarifa hizi na asifurahie kabisa maisha ya Madrid akiwa chini ya kocha huyu ambapo kocha huyu ameonekana anapenda sana wachezaji wenye nguvu na wanaojitoa na walio na ufanisi wa mbinu tofauti tofauti.

Sijamaanisha kwamba Winga huyu wa Welsh eti ataofanikiwa chini ya kocha huyu na kama akijbakia Bernabeu atajikuta anapewa majukumu ya kucheza katikati na pia ni taarifa mbaya kwa maveterani kama Cristiano Ronaldo, Marcelo, Luka Modric na wengine wengi na Lopetegui yupo teyari kuwaweka wachezaji vijana zaidi kuziba hizi nafasi huaga ata achagui.

Image result for karim benzema

Kareem Benzema mtu aliekuwa anambeba hayupo kwasasa unazani hii ndio itakuwa njia kwake ya kuondoka najua Ubora wake kwenye mpira ni kitu ambacho Lopetegui atakikubali na atajirekebisha kwa yale makosa aliokuwa anafanya mimi binafsi nina Imani na hiyo kitu.

No comments:

Post a Comment

Pages