Malikia wa RNB Duniani Ashanti amethibitisha siku ya Jumapili kwenye tuzo za BET awards kwenye red Carpet kwamba yeye na rapa Ja Rule wana mipango ya kurekodi album mpya kwa pamoja.
Na hii ilianza baada ya Ja Rule kutupia picha kwenye mtandao wa Instagram inayowaonesha Beyonce na Jayz na kuandika "Iconic..The Carters..New album is dope!!! I think we should do one these joint albums hahah.."

Kwa pamoja Ashanti na Ja Rule waliweza kufanya vizuri mwaka 2000 ukiunganisha vibao kama "Always on Time" "What's Luv?" wakiwa pamoja na Fat Joe bila kusahau "put it on me" na nyingine kibao.
No comments:
Post a Comment