'TUTAONA' Eden Hazard amewatadharisha Chelsea ataondoka labda klabu ifanye usajili mkubwa msimu ujao. - BZONE

'TUTAONA' Eden Hazard amewatadharisha Chelsea ataondoka labda klabu ifanye usajili mkubwa msimu ujao.

Share This
Eden hazard ameleta mshtuko mkubwa kwenye klabu ya Chelsea kwa kutaka klabu yake ifanye usajili wa maana au aondoke.Hazard mwenye umri wa miaka 27 bado anasubiria  kuweza kutia wino kwenye kandarasi ya mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki ila kwanza aone nini kitachoendelea kwenye dirisha la usajili.Mbelgiji huyu anamiaka miwili amebakiza kwenye dili la makataba wake lakini Real Madrid wanasubiria ili kufungua mabawa yao.Alitahadharisha, "Bado ninasubiria. Ninasubiria wachezaji wapya msimu ujao. Tutaona. Mimi ninataka wachezaji ninataka kuona tunabeba kombe la ligi msimu ujao  na mengine. Ni kitu kikubwa sana  kwahiyo nitaitaji kufikilia sana vitu vingi."

Eden Hazard

Kocha wa wanadarajani Antonio Conte aliweza kuvunja rekodi darajani kwa kufanya usajili wa Pauni Milioni 65 kwa mshambuliaji Alvaro Morata kati ya moja ya manunuzi kwenye Pauni 250m mwaka wa jana.Kikubwa anachohofia Conte ni kumpoteza Hazard kwasababu anausawishi mkubwa darajani lakini ikumbukwe Hazard pia msimu ujao atoweza kucheza klabu bingwa Ulaya kwasababu klabu yake imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 5.

No comments:

Post a Comment

Pages