Nina uhakika aitokushangaza kusikia eti Manchester United wamelikosa kombe la FA, ngoja tujipe matumaini kwamba United watalibeba kombe la FA na Rafiki yetu kijana wetu Cristiano Ronaldo atapata hat-trick ya UEFA, japo Liverpool wamejitahidi sana kufika hadi kwenye fainali za klabu bingwa Ulaya.
Ila kwa topic tuliokuwa nayo hapa kwa united jinsi aina ya uchezaji waliokuwa nao chini ya kocha Jose Mourinho na jinsi tukijaribu kulinganisha na Sir Alex Ferguson kwasababu yeye alikuwa ni funguo alikuwa akija kila msimu na silaha za hatari ambazo zilikuwa hazina ata majina.
Chini ya David Moyes, Louis Van Gaal na Jose Mourinho watu wamekuwa wakisema kwamba soka la United sio zuri na kila mchezo ambao alikuwa akicheza Ferguson siku hadi siku ulikuwa mzuri kwasababu anakufanya usahau michezo mibaya iliopita na kupoteza michezo ambayo uwezi tarajia.
Mimi nadhani sisi mashabiki wasasa tunajifanya mahodari sana kwenye kufikilia kuhusu mpira tunasahau kipindi cha Ferguson na ile michezo ambayo tulikuwa tunatamani hata kujiua.
Ndio..!! kilikuwa ni kipindi kigumu sana lakini kutokea 2003 mpaka 2006 haikuwa vizuri kabisa walikuwa mafundi kibao lakini hawakuwa vizuri hawakucheza kile kiwango cha juu tulichokuwa tunakitaka mashabiki, nazani unaweza ukaona ni jinsi gani tunajaribu kupima kile kipindi cha nyuma na sasa na kumbuka kile kipindi Jose alipokuwaa Chelsea na alikuwa akituteketeza kabisa.
Kiukweli City msimu huu ata mimi wamenishangaza sana hasa pale walipokuwa wakijichukulia alama tu na hapa ndio tunaona kitu kinaitwa pure football jinsi city na United wanavyocheza ni tofauti kabisa lakini Manchester United walijua kwamba tukimchagua Mourinho na City lazima watamvuta Guardiola.
Inaonekana ni kama sauti ya kujilinda kwasababu ndio ilivyo, Mimi nina amini kwamba lazima Mourinho abebe kombe la kwanza la ligi tangia Ferguson aondoke mwakani anaweza akajiandikia jina kwenye vita vipya. Makocha hawa wote wawili walipokuwa Real Madrid na Barcelona wote waliweza kubeba mataji ya ligi
Home
Unlabelled
Mashabiki wa Manchester United wamesahau jinsi gani walivokuwa vibaya 2003 mpaka 2006.!
Mashabiki wa Manchester United wamesahau jinsi gani walivokuwa vibaya 2003 mpaka 2006.!
Share This
Share This
About Bwherever
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Bwherever is a Tanzanian Radio Personality and Blogger who initiative Bbaseonpoint blog.
No comments:
Post a Comment