MH..!! kuacha Pombe ni kweli? Prezzo kuzichukia Pombe. - BZONE

MH..!! kuacha Pombe ni kweli? Prezzo kuzichukia Pombe.

Share This
Msanii wa Hip Hop kutoka Kenya, ametoa ujumbe wa kushtua kwa mashabiki wake baada ya kusema kuwa anazichukia pombe.


Kupitia mitandao ya kijamii, Prezzo anayependa kujiita Mfalme wa Ming’aro aliwaambia mashabiki wake hasa wanaume kuwa makini katika maamuzi yao. Aliwaasa kutumia pesa zao wanazopata vizuri kwa wanawake na pia katika matumizi ya pombe.


“Usipende kutumia pesa yote kwa wanawake, watakutoa ufalme. Mfalme hatakiwi kunywa wine au pombe kwa sababu anapokunywa lazima asahau sheria na mahitaji ya mtu. Pombe zimeletwa kwa sababu ya kupoteza malengo, umasikini na kutokuwa na furaha. Nimemaliza! Ubarikiwe.”


Baada ya kuandika hivyo, mashabiki wake wengi walimjia juu na kumtaka aseme kama anayosema anamaanisha na kweli ameacha pombe ambapo alisema, kwa sasa anakunywa vinywaji laini tu.

No comments:

Post a Comment

Pages