Fahamu aina 5 za Sneakers ambazo zitakufanya uwake Ikiwemo Air Jordan 1 Homage To Home na zaidi. - BZONE

Fahamu aina 5 za Sneakers ambazo zitakufanya uwake Ikiwemo Air Jordan 1 Homage To Home na zaidi.

Share This
Weekend ilishaanza kukiwa na Sneakers kali..! kukiwa na idadi kubwa ya Sneakers lakini usipitwe na hizi mbili ikiwemo na toleo jipya kutoka Nike, Adidas na Jordan.

Related image

Kukiwa na ukali wa Moto hizi hapa aina tano za Sneakers ambazo nimekuokotea leo tukianza na Jordan 1 Retro Homage to Home, Nike Air Max 270 Camo Sunset, Adidas Alexander Wang Aw Reissue Run, Nike Air More Money Court Purple na Skepta x Nike Air Max 97/BW.

Related image

Kupitia Jumpman imezndua Air Jordan 1 Homage To Home ikiwa chini ya Micahel Jordan ambapo toleo ili aliweza kulitumia kwenye mwaka 1998 ikiwa inajulikana kama Jordan 1 Classic Colorways lakini sasa hivi imekuja ikiwa na maboresho kidogo ikiwa na thamani $190 sawa na 431,000/= za kitanzania  hizi AJ 1 zinapatikana kwasasa nje ya Bongo lakini unaweza ukazipata kupitia mawakala wa Nike Duniani kote.

Image result for Nike Air Max 270 Camo Sunset

Bzone imekuchukulia Sneakers kali zenye thamani kubwa Duniani huku Nike wakitoa kiatu kingine walichoshirikiana na Rapa mzaliwa wa London yani skepta. Hybrid  Sneaker inavitu kama ilivyo Air Max 1 na Air Max 97 Hizi karibia zitakuwa sokoni mda si mrefu  huku thamani yake ikiwa $120 na $250 sawa na 272,400/= na 567,500/= za Kitanzania.

Image result for Nike Air Max 270 Camo Sunset

No comments:

Post a Comment

Pages