Kwani ni Kweli Ngoma Hakuwa mgonjwa kivile, au alifanya hivi ili kurahisisha safari yake..? - BZONE

Kwani ni Kweli Ngoma Hakuwa mgonjwa kivile, au alifanya hivi ili kurahisisha safari yake..?

Share This
Alijua fikra kama bado anamkataba na Yanga ata kama angecheza ingekuwa ngumu sana kwake kuvunja na ndomana akatumia ujanja ujanja wake anaoujua yeye.



Mshambuliaji huyu wa zamani wa Yanga akijulikana kamaDonald Ngoma ambae jana imetaarifiwa kwamba ameweza kujiunga na klabu inayoshiriki Ligi kuu ya Tanzania Bara Azam Fc ambao wanaotokea kwenye dimba la Chamazi japo Mzimbabwe huyu aliamua kufanya hivi wakati kila mtu anajua bado ana mkataba na Yanga na Japo aliweza kutupa ahadi zisizo na ukweli ndani yake.



Akiwa amekabidhiwa jezi namba 11 ile ambayo alikuwa akitumia kwa watoto wa Jangwani, Ebu ngoja nikuulize imekuaje Azam wamekubali kumchukua Ngoma ambaye ni majeruhi wa mda mrefu na ajaweza kucheza almost michezo Mingi kwenye Ligi wala michuano mingine na Yanga kwa haraka haraka tu ilo haliwezekani..!! Lazima kutakua na mchezo hapa kati japo tunasikia wamekubaliana pande zote mbili yani mchezaji na Klabu aliyoweza kutoka.

Image result for donald ngoma

Na kwa taarifa tunazoendelea kuzipata eti Hans Van Der Pluijm ambaye aliewahi kuifundisha Yanga na kufanya kazi na Mzimbabwe huyu inaonekana mda wowote kuanzia sasa anaweza akajiunga na kikosi cha Azam FC na alichoweza kuwaambia ni kwamba wanatakiwa wahakikishe wanamsajili Donald Ngoma kutoka Yanga huku Klabu aliyopo sasa Singida United wameshatangaza kuachana na Kocha huyu japo walima halizeti wanachosubiria kwa sasa ni kumalizana na Fainali FA dhidi ya Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment

Pages