Kwani ni kweli Kiba alitelekeza Mtoto? - BZONE

Kwani ni kweli Kiba alitelekeza Mtoto?

Share This
Alikiba amefunguka na kusema kuwa amesikia na kusoma mitandaoni na kwenye magazeti kuhusu malalamiko ya mzazi mwenzie, Hadija kwamba ametelekeza mtoto wao lakini bado hajapata barua rasmi kutoka mahakamani.

Akipiga stori na Kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Kiba amedai mzazi mwenzake huyo aliinyanyasa sana familia yake kwa sababu alikuwa hataki kabisa mtoto aishi kwa upande wa wazazi wake.


“Mtoto nilikuwa namlea vizuri tu, kila wikiendi alikuwa anakuja nyumbani na kama kumuhudumia natimiza majukumu yangu, sijajua sababu ya mwenzangu kuniletea fujo ila sijawahi kupelekwa Polisi.

“Mimi niliiona kwenye gazeti, hayo malalamiko yapo Ustawi wa Jamii, haya yalitokana na mama yule alivyokuwa akitunyanyasa sisi sote familia yetu kuuhusu kukaa na mtoto ama kumuona.


“Sasa kwa kuwa mtoto naye ana haki na anatamani kumuona baba yake, unamwambia leo Ijumaa mlete mtoto aje kukaa huku hadi Jumapili atarudi kwa ajili ya shule Jumatatu, cha kushangaza tukimchukua mtoto Ijumaa, siku hiyo hiyo au Jumamosi anakuja kumchukua anadai heti anam-miss, binafsi sikuweza namuelewa kabisa,” amesema Alikiba.

Aidha, Alikiba amesema amefurahi kuitwa mahakamani kwani haelewi mpaka sasa lengo la mzazi mwenzake huku akidai kuna kipindi mtoto anafikia hadi hatua anataja jina lingine la baba yake kitu ambacho kilimfanya aache kutoa huduma kwa mtoto.

 

“Mimi nilikuwa nataka ifike huko ilipofika (Mahakamani), sababu haiwezekani kama kumuhudumia mimi nilikuwa namhudumia tena vizuri tu. Mtoto nimemtoa kwenye shule aliyokuwa akisoma, nikampeleka shule ya gharama zaidi ya mara tatu ya ile aliyokuwa akisoma mwanzo. Sasa yanapotokea haya nashindwa kuelewa lengo lake ni nini?” amesema Alikiba.


Ikumbukwe kwamba, wiki iliyopita taarifa zilisambaa kuwa Alikiba ameshtakiwa katika Mahakama ya kisutu na mwanamke mfanyabiashara ya mitumba, ambaye ni mzazzi mwenzake, Hadija akidai kuwa msanii huyo ameshindwa kumhudumia mtoto wao kinyume cha taratibu.

No comments:

Post a Comment

Pages