J.cole mzizi wake wa kuandika hadithi uliweza kukulia na kutokea kupitia Tupac Shakur, OutKast, Jay-z, Nas na Eminem. kwahiyo kihalisia uwezo wake wa kuandika ulitokana na hawa watu jinsi ya kupangilia maneno hii inamaanisha mziki upo damuni. Cole amejaribu kukuza na kujipa uwezo wa kutoa shukrani kwa haina yake kwa maisha aliyoweza kupitia na kujitoa muanga kupitia mambo mbali mbali Cole.
Lakini pale inapokuja kwa historia ya Cole akuweza kujipa mipaka anaweza akakuambia kitu ambacho ukuweza kukitarajia kukipoteza kama kwa mwanamke alie bikra na kupoteza bikra lake ebu jaribu kuisikiliza "Wet Dreamz" hakuna alietarajia kama angeweza kuchana juu ya kutoa mimba jaribu kuisikiliza "Lost ones" Uhodari wake na kipaji chake cha kuhesabu hizi historia labda uzito wa jambo kutokana na malika yaliokuwepo kwasababu kila neno limechaguliwa kikamilifu.
Cole anaendelea kutuonesha kuna mambo kapitia na atutakiwi kukata tamaa ata kidogo kazi hii ameionesha kupitia kwenye KOD ikiwa ni album yake ya tano ambayo imewekwa umahiri mkubwa sana, kukiwa na mistari iliyonolewa kisawa sawa huku kwenye album yake nzima ikiangalia kwa umakini baadhi ya vitu ambayo inatupa tahadhari kwenye maisha Historia kutoka kwenye KOD inagusa kila kitu kinachokuwepo kwenye maisha ya sasa ya utandawazi.
Hizi hapa nyimbo 20 ambazo ukipata mda wa kuzisikiliza ndio utajua nini kinachongelewa na J.Cole
"03 Adolescene"
Hii inatuambia historia ya J.cole alipotokea sio kwenye Mziki lakini inachungulia maisha ya ukubwani aliyopitia. Akiwa na miaka 18 Cole alikuwa yupo teyari kwenda chuo cha St. John lakini akili yake ilikuwa imenasa katikati kwa status yake ilivyo nyumbani akiwa na matumaini ya kuingia kwenye madawa ya kulevya na ndio yatamtoa kimaisha. Alijaribu kupata mazungumzo kidogo na rafiki yake wa nyuma huko kidogo na akamwambia ;Nigga you know you sound right now? if you wasn't my friend i would Crown you right now."
"3wishes"
J.cole anachukua pembe nyingine kwa kutuambia historia nyingine na kutuelezea kwamba nini angeweza kufanya kama angekuwa sio binadamu nani angempa matumaini matatu, wakati unaendelea kutarajia kwamba rapa huyu angejitabilia tumaini yeye binafsi na kuwa na mafanikio na utajiri wa haina yake kwenye rap game.
"4 your Eyez Only"
Ngoma hii inaelezea dakika tisa ambazo cole anazichukua binafsi kwa rafiki yake alieweza kupoteza maisha na kuacha audio ya maneno ambayo yamfikie mtoto wake.
"Breakdown"
Kwenye ngoma hii Cole anajaribu kumkumbuka Mariah Carey alipoachiaga ngoma yake ya Breakdown mwaka wa 1997 ambayo inaelezea storia binafsi, kwenye verse ya kwanza inakuta Cole uso kwa uso na baba yake ambaye haeleweki huku verse namba mbili niamuangazia mama yake akiwa ametaaliwa na madawa ya kulevya na ya tatu ikimchukua yeye mwenyewe binafsi akikamatwa mahusiano ambayo yanampelekesha kuwasahau hadi wazazi wake.
"Chaining Day"
Humu Cole anatuchana kuhusiana jinsi yeye alivoweza kupigania unyakinifu na anakuja kujikuta kwamba anaishia kwenye maisha ya udanganyifu.
"College Boy"
kwenye hii tunamuona Cole ambae ni msomi lakini mkorofi yeye kila mwanamke chuoni anataka kuwa nae kwenye mahusiano lakini akiwemo kwenye timu ya mpira wa kikapu akiwa na ndoto kubwa za kuwa mwanakikapu maarufu Marekani.
"Crunch Time"
Hapa anamuongelea rapa ambae alikuwa mpambanaji lakini alikuwa nasubira kwenye ndoto zake akuzifanyia haraka.
"Dreams"
Humu Cole amejaribu kusample kutoka kwa Kanye kwenye ngoma ya Drive slow ikiwa inamuelezea mwanamke ambae anataka kukatiza ndoto za Cole.
"Is she Gon Pop"
Chin ya dakika 3 Cole anakaaa chini anajaribu kupaka rangi stori hii kuhusu wanawake ambao wapo makamo fulani hivi na kulala na nyota mbali mbali wakijua kwamba ndoto zao zitaenda kukamilikia hapa.
"Killers"
Akiimba kwa mara ya kwanza kwenye mauaji, Cole anaomba msamaha kwa mama yake na anajilinganisha jinsi yeye kwa sasa na watu anaowapenda na anajaribu kutuambia kwamba maisha ni kama filamu.
"Land of the Snakes"
Hapa anatuelezea jinsi alivoweza kuhamia kwenye mji wa Los Angeles akiwa na rafiki yake wa chuoni Cole anaonesha usaliti kwa marafiki na tabia zisizo nzuri na ambazo azifai kwenye jamii.
"Let Nas Down"
Kwenye ngoma hii ya Nas down Cole amejaribu kutuonesha mashujaaa wa kwenye game ya Hip hop na nini maana halisi ya mziki wa hip hop.
"Lights Please"
Hii ndio nyimbo ambayo imemuweka Cole kwenye ramani, na hii ameonesha nini maana ya sanaa kupitia mziki na msaada wake kwenye jamii lakini imeweka kwa ukaribu mapenzi na kumuonesha mtu ambaea anataka kufanya mapenzi.
"lost Ones"
J.cole ameshinda kwenye kupata wasikilizaji na kukusanya mioyo yao kwenye maswala ya utoaji mimba.
"Neighbours"
Hapa Cole ameonesha tukio alilokutana nalo mwaka 2016 lilotokea Kusini mwa Carolina Airbnb ambapo polisi aliweza kumua Jirani yake.
"Once an Addict-Interlude"
Kwenye Kod Cole anajaribu kuzama mpaka kwenye giza kwenye ukurasa wa maisha yake muingiliano wa pombe ambazo zilimuingia mama yake kichwani ambapo waliishi pamoja na kupelekea maisha kuwa magumu sana.
"Runaway"
Humu Cole anaendelea kupambana na maigizo yaliokuwemo kwenye maisha akiwa na mawazo lukuki na yaliokuwa na imani ndani ya moyo wake.
"School Daze"
Simple tuu J.cole anajaribu kuangalia nyuma kipindi cha maisha alipokuwa shule akiwa Hopeful rapa ambae ambae atakuja kuwa na Ela, Wanawake na mambo kibao kwenye kichwa cahke na shule anaona kama si kitu.
"The Storm"
Tupa nyuma kidogo kipindi kile Cole alipokuwa anajulikana kama Therapist alikuwa mdogo na mwenye sauti hatari sana ikiwa mvumo wa radi kama ile ya Ali Kiba, anaelezea stori ya Shawn na Nina wapenzi wawili ambao walichezea sana penzi lao kuishia wakizinguana.
"Wet Dreamz"
Ngoma hii imemlenga tena au sana mwanamke ambae amekamilika kila idala nazani unanielewa lakini japo amekamilika kwa kila kitu msichana huyu anachezea uzuri wake vibaya na kumpa mawazo yalioweza kuloana.
Home
Unlabelled
Hizi ndio kali 20 za J.Cole ambazo za kukuliwaza.
Hizi ndio kali 20 za J.Cole ambazo za kukuliwaza.
Share This
Share This
About Bwherever
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Bwherever is a Tanzanian Radio Personality and Blogger who initiative Bbaseonpoint blog.
No comments:
Post a Comment