Ebu achana na NickMinaj ata Cardi B na wengine kibao, Ila Dej Loaf nimejaribu kumsikiliza siku Moja I WONDER kwanini hawamsikilizi? - BZONE

Ebu achana na NickMinaj ata Cardi B na wengine kibao, Ila Dej Loaf nimejaribu kumsikiliza siku Moja I WONDER kwanini hawamsikilizi?

Share This
Siku moja katika pita pita zangu nilipata kusikia nyimbo moja kutoka majuu ikipigwa kwenye Duka moja huku nikimsikia mwanadada akirap kwa sauti ya aina yake..Umh nikajiuliza ni nani huyu Nah sikutaka kupita Bure nikasogea kumsikiliza vizuri na nikauliza hii nyimbo inaitwaje ndipo nilipoambiwa ni 'DESIRE' hiyoo..!!

Related image

Nikajipa mda kidogo wa kujiuliza baadhi ya maswali kwenye kichwa changu moja ya swali ambalo lilikuwa kwenye kichwa changu ni kumbe Ulaya kama Bongo tuu sio wote wanaosikika kwenye ramani ya mziki japo wanajua tatizo ni nini sasa Airtime au? Maana msaniii kama huyu tena kutoka nchi za Magharibi ina maana hana Management hapana bhana.

Image result for dej loaf

Kwa haina ya mziki anayo fanya na kwa mtindo anaotumia kwenye kurap ananitupa nyuma ya kapu na kuanza kunikumbusha kipindi kile cha miaka ya 90....

Anajulikana kama Deja Trimble au unaweza ukamuita Dej Loaf ni rapa huyu wa Kimarekani lakini kwa uwezo wake wa kuvunja vyuma kwa sauti yake ndio kilichonivutia juu yake ata pale nilipomsikia kwa mara ya kwanza alinikaa sana kwenye masikio yangu na Moyo wangu, Rapa huyu sio wa leo kwasababu alianza kufanya ishu zake za kimziki tokea 2011 japo aliweza kujulikana sio kwa kiundani sana mwaka 2012 pale alipoachia ngoma yake ya JUST DO IT.

Image result for dej loaf

Rapa huyu aliweza kujipatia baadhi ya mafanikio ikiwemo kibao chake cha Try me asee kibao hiki kiliweza kuwakamata watu karibia Dunia nzima na kuvunja baadhi ya rekodi kama kwenye Jarida la XXL MAGAZINE Freshman pamoja na kushika baadhi ya nafasi kwenye chat ya Billboard,

Nilijaribu kumcungulia hivi ni kwanini hayupo kama marapa wengine wakali wa kike tunao wasikia..? Ila yeye binafsi ana amini kwa kile anachokifanya na anacho kipata Dej baada ya kibao chake cha TRY ME kutoboa akajikuta anaacha kazi.

Image result for dej loaf

Nina kwambia hivi ni amini mimi ukimwangalia kwa haraka haraka ata kabla ajaimba mtu yeyote anakuwa teyari ameshapata jibu kwa kile ninachokisema Kupitia chombo kimoja cha Marekani Loaf aliweza kufunguka na kusema baadhi ya maneno 'Kama ingekuwa mziki wangu unasikika kipindi cha kina Pac ningekuwa ni tofauti kabisa' Hapa ndipo nikamuelewa rapa huyu anaonglea real life in Music na unyanyasaji watu wanaoupata kwenye jamii zetu tofauti.Haikuwa rahisi kwake yeye mpaka kufika hapo alipo kwasasa kuweka mzike kwenye mtandao na kusikilizia sio kitu kidogo hiko yataka Moyo asikwambie mtu nazani sasa ushaanza kuelewa nini ninachokiongelea juu ya rapa huyu, ila niruhusu nikwambie hivi 'HER WORDS ARE TOUGH AND HER VOICE IS SWEET A SOUL AS HER HEART' Mziki its all about Real Life usifanye mziki ilimradi upite masikoni mwetu tu.

No comments:

Post a Comment

Pages