Anachukua nafasi ya David Moyes ambae ametolewa na klabu baada ya mkataba wake kumalizika baada ya kushika nafasi ya 13 kwenye Ligi. Moyes alipewa Ofa ya dili jipya kati ya wiki nne zilizopita ambapo ikampelekea kuachia ngazi.

Pellegrin ataungana na klabu hii ya London akiwa na msaidizi wake wa kuaminika yani Ruben Counsillas West Ham walikuwa na matumaini ya kuwanasa makocha tofauti tofauti kabla kunasa sahihi ya Mchile huyu akiwepo kocha wa Newcastle United Rafa Benitez.
Pellegrin baada ya safari ndefu sasa anarudi Kwenye Ligi kuu ya Uingereza akitokea nchini Chini lakini bado atabakia kuwa ni kocha ambae atakuwa analipwa mshahara ambao upo juu, aliweza kunyakua kombe la ligi akiwa na City kwenye msimu 2013-2014 huku akitumia miaka mitatu akiwa na City kwenye dimba la Etihad na bado, pia anakumbukwa na mashabiki wa City.
No comments:
Post a Comment