Mashabiki wa Arsenal walijua tu kama hili litatokea lakini sio kuondoka kwa Santi Cazorla msimu huu.
Akiwa nyuma ya kivuli cha Arsene Wenger baada ya miaka 22 akiwa anaongelea mafanikio yake kwenye dimba la Emirates huku tukiwa tunamuona aliekuwa kocha wa PSG akikaribia kuchukua mikoba ya Wenger yani Unai Emery amefanya habari za Cazorla kuondoka kuekwa chini ya kapeti kimya kimya.
Muhispania huyu inasemekana anaweza akarudi kwenye klabu yake ya zamani yani Villarreal huku Cazorla akijikuta kwenye wakato mgumu baada ya kupatwa na majeraha ya mda mrefu na kumpelekea namba yake au nafasi anayocheza kushikiliwa na watu wengi klabuni hapo.
Kwani kiungo huyu wa Arsenal mwenye kipaji cha aina yake kwani ni mzuri kuliko Samir Nasir au ni mzuri kuliko Mesut Ozil au Cesc Fabregas ambae aliondoka bila kuhurumiwa na shabiki yeyote.
Cazorla alitua kwenye msimu wa 2013 huku akiipa faida kubwa klabu ya Malaga kwa kifedha kwa kufanya kuweza kuwavuta na Nacho Monreal kwa dau lile lile linalotaka kukaribiana.
Mbali na majeruhi yake kiungo huyu alishatuonesha ubora wake upo wapi pale London kaskazini akishilikiana vizuri na Jack Wilshere, Aaron Ramsey na Mikel Arteta. Mbali yakuwa na futi 5 pamoja na inchi 6 za urefu Cazorla alichukua nafasi kubwa kwenye Ligi ya Uingereza kwa mtindo wake wa kucheza soka aliokuwa nao huku akiwapa changamoto viungo wengine aliokuwa akichuana nao toka timu pinzani na kutengeneza nafasi nyingi kwa wachezaji wenzake.
Jinsi ya Uhalisia wa Pasi zake ilikuwa ni Neema kwa Arsenal Cazorla ndio alikuwa jibu pekee kwa David Silva wa Manchester City na akiwa mtu pekee wa katikati kati ya Ozil na Fabregas. Lakini baada ya Ozil kutua Arsenal Cazorla alioneka kushuka kiwango lakini kwenye michezo yote muhimu ya Arsenal alikuwa akitegemewa.
Kuondoka kwake kutatuuzunisha tulio wengi na dhairi anaonekana kumfata nyuma Wenger ila akumbuke atakumbukwa sana mbali alikuwa na majeraha ya mda mrefu.
Home
Unlabelled
Cazorla alikuwa ni Moja ya viungo pendwa ambae soka lake lilikuja kupotea kwa majeraha, kuondoka kwake kumetuachia majonzi makubwa sana..!!
Cazorla alikuwa ni Moja ya viungo pendwa ambae soka lake lilikuja kupotea kwa majeraha, kuondoka kwake kumetuachia majonzi makubwa sana..!!
Share This
Share This
About Bwherever
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Bwherever is a Tanzanian Radio Personality and Blogger who initiative Bbaseonpoint blog.
No comments:
Post a Comment