Mbelgiji huyu amekuwa kwenye rada za Real Madrid kwa miaka kadhaa akitazamiwa kuwa mrithi wa Cristiano Ronaldo.
Sasa hiyo inataarifiwa inaweza ikabadilishwa mda wowote huku Real Madrid wakiwa kwenye hofu kubwa ya kutumia pauni milioni 100 kwa nyota huyo wa chelsea wakiofia mchezaji huyo ameshuka kiwango na watakaa kumtazama mpaka pale kombe la Dunia litakapo malizika.
Mbali na hiyoo nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa sehemu muhimu ya Muitaliano Antonio Conte huku Chelsea wapo teyari kupokea ofa ya pauni milioni 100 kwa timu yoyote itakayo mtaka mchezaji huyoo.
Chelsea nao pia wanajiandaa kuandaa Ofa kwajili ya mshambuliaji kinda wa Real Madrid Marco Asensio lakini kwa upande mwengine Chelsea wataendelea kumkazia Hazard ili aweze kuongeza mkataba na wapo teyari kumfanya kuwa mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa ndani ya Chelsea kwa kulipwa pauni 300,000 kwa wiki akitokea pauni 200,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment