
Klabu hiyo ya London inatafuta wagombea ambao wataweza kuchukua mikoba ya babu Arsene wenger ambae amekuwa na msimu mgumu sana.
Nafasi ya nne kwenye Ligi haitoweza kupatikana kwasasa na kituu pekee kilichobakia kwa Arsenal ni ushindi dhidi ya timu pendwa sana Duniani kwasasa Atletico Madrid ambao wanaenda kukutana kwenye hatua ya nusu fainali ambapo ndio njia pekee kwa Arsenal kuweza kwenda kwenye klabu bingwa Ulaya. Kumekuwa na kelele nyingi sana kutoka kwa mashabiki kwenda kwenye klabu na Wenger ambae wanataka aachie nafasi hiyoo na amekua kocha wa timu hiyo kwa mda wa miaka 22 mpaka sasa.

Gwiji huyu ambae alikuwa kiungo wa zamani wa Arsenal ambae kwasasa anamiaka 41 kwasasa ni kocha wa klabu kutokea marekani ikijulikana kama New York City na bado anamkataba na klabu ya Manchester City akiwa kama balozi wa klabu hiyo.

Appointment yake hiyo ya kutaka kuwa kocha wa klabu yake ya zamani inawashtua mashabiki wengi ambao hawataki Vieira kuchukua nafasi hiyo kwa tuhuma ya kuwasaliti. Aliweza kushinda mataji matatu ya ligi kuu na akiweza kubeba mataji matatu ya FA kabla ya kutimkia kwenye klabu za Juventus, Inter Milan na Manchester City ambapo aliweza kushinda kombe la FA mwaka 2011.
Na hakaweza kutumkia kwenye hatua ya ukocha ambapo alifanya kazi kwa miaka miwili akiwa pale City kwenye upande wa kukuza kikosi kabla ya kuchukua ukocha mkuu mwaka 2016 alipoichukua klabu ya New York City kwenye ligi ya MLS.
Kwasasa kwenye klabu ya Arsenal hakutokuwa na mabadiliko yoyote makubwa kwenye benchi la ufundi kama hatataka kurudi. Mbali na hiyo kocha Arsene Wenger atoweza kufukuzwa hata kama hatochukua kombe la Europa ligi.

Kocha huyu mwenye umri wa miaka 68 kwasas aliweza kuweka sahihi ya miaka miwili kwenye kandarasi aliyoweza kupewa baada ya kunyakua kombe la FA kwa kuibamiza klabu ya Chelsea na uhamuzi wa kuondoka hanao yeye mwenyewe.
Anamahusiano makubwa na mmiliki wa klabu hiyo ambae ni Bilionea kutokea nchini Marekani akijulikana kama Stan Kroenke ambapo na yeye ana hisa kadhaa kwenye klabu hiyo ya washika mitutu.
No comments:
Post a Comment