

Kiungo huyu wa Uingereza amekuwa na mchezo afifu dhidi ya CSKA Moscow kwenye michuano ya Europa kwenye hatua ya robo fainali hasa kwenye mzunguko wa pili ambapo Arsenal wameweza kutoka sare ya 2-2 na kufanya wasonge mbele kwa jumla ya magoli 6-3.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Keane ametupia jiwe Wilshere kwa kusema hana kiwango chochote na amepungukiwa uwezo wa kusambaza mipira kwajili ya ushambulizi na amefunguka kwa kusema siku zijazo anaweza akaachwa kabisa.
Keane aliweza kusema ‘Kama wewe ni mchezaji mkubwa Duniani lazima uwe fiti mda wote na kila mda napomuona lazima atibiwe au anatolewa kabisa.’
‘Sijawahi kuwa shabiki yake mkubwa sana kwa mchezaji ambae ni mshambuliaji alafa apati magoli ya kutosha au usaidizi wowote kwa wenzake. Huyu jamaa soka lake linaisha, na sipendi kulioba hili kutoka kwake kama Arsenal ilovo mbaya na yeye mwenyewe ndivyo alivyo.’
‘Kwani teyari kashapewa ofa ya mkataba mwingine? Kama mimi ningekuwa yeye ningesaini tena kwasababu kama anafikilia atapa ofa kubwa kwenye vilabu vikubwa msimu ujao asahau ilo. Swali kubwa kuhusu yeye kwenye kile kikubwa anachokikosa na ambacho ajawahi kukipata.’

Wilshere amekuwa akisimbuliwa na majeruhi kwa mda mrefu sasa na alienda chini kwenye mchezo uliokuwa unachezwa Urusi jana kwa jili ya Enka kabla ya kufanyiwa mabadiliko kwenye dakika ya 69.
No comments:
Post a Comment