HANA FURAHA..! ANTHONY MARTIAL ANATAKA MAZUNGUMZO YA KWENDA ARSENAL, IKIWA NI SEHEMU YA DILI LA SANCHEZ. - BZONE

HANA FURAHA..! ANTHONY MARTIAL ANATAKA MAZUNGUMZO YA KWENDA ARSENAL, IKIWA NI SEHEMU YA DILI LA SANCHEZ.

Share This
Mshambuliaji wa Manchester United ametaka mazungumzo ya kwenda Arsenal yaanze kutokana na ripoti kutokea The Times.



Mfaransa huyu inasemekana hana furaha kabisa akiwa Old Trafford na amekuwa akiusishwa na uhamisho wa kwenda Juventus na Bayern Munich kwenye wiki zilizopita.



Mshambuliaji huyu akuweza  kuanza mchezo wa Ligi kuu tangia ushindi waliopata wa 2-1 dhidi ya Chelsea mwezi wa Februari kwenye mechi tisa za nyuma kwenye mashindano ya klabu.



Na ripoti zinashtaki kwa kusema amekuwa hana furaha kwa kuto ruhusiwa kuzungumza na washika mitutu pale alipotajwa angekuwa ni mmoja kati ya mabadilishano na Arsenal mwezi wa Januari kwenye dirisha dogo la usajili ambapo tulimuona Alexis Sanchezakitoka Emirates na kuelekea Old Trafford.

Martial mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na United akitokea Monaco mwaka 2015 kwenye dili la Pauni milioni 58 lakini amekuwa hapati nafasi kadhaa kwenye kikosi cha kwanza mbali na kupendwa na mashabiki.



Kwenye mzunguko wa kwanza msimu huu Jose Mourinho alikuwa akifanyiwa mabadiliko yeye na Marcus Rashford kwenye eneo la ushambuliaji lakini tokea atue Sanchez ambae ameshinda magoli mawili mpaka hivi sasa  akiwa na michezo 13 na amekuwa akiwaumiza vichwa washambuliaji wadogo.

No comments:

Post a Comment

Pages