Aliekuwa mchezaji wa zamani wa Brazili Roberto Carlos amesema Neymar anatakiwa kuwa na subira kama anataka kuchukua ballon d'or kwasababu Messi na Ronaldo bado wazuri.
Tumeweza kuona Neymar amezidi kupata eshima kubwa hasa pale alipo hamia PSG msimu huu huku akiwa anajiandaa kuweza kushiriki kombe la Dunia miezi michache inayokuja japo kwasasa yupo kwenye kujitibia na majeruhi yanayomkabili.
Kwasasa ndio mchezaji ghali Duniani Neymar ameshinda magoli 26 kwenye michezo 29 msimu huu akiwa na uhamuzi mgumu wa kuondoka Barcelona.

Carlos ambae alishinda akiwa na Brazili kwenye mashindano ya kombe la Dunia mwaka 2002 alifunguka na kusema "Ninafikilia amefanya jambo la maana kusaini PSG.
"kuwa mchezaji mzuri Duniani tulitaka kuondoka Barcelona kwanza kwasababu ya pale kuna Messi,
Licha ya hivyo anatakiwa kukaa kwa tahadhari na akijua kwamba pale anapokuwepo Messi na Ronaldo tena bado wapo kwenye kiwango itabidi avumilie kuwepo nafasi ya tatu."
Neymar bado anaendelea kuhusishwa na uhamisho wa kudondoka Real Madrid msimu huu lakini kwasasa anafikilia kuwa fiti ili kuweza kukipiga kwenye kombe la Dunia.


No comments:
Post a Comment