MAMA AISHI KWENYE KONTENA MTOTO ANACHEZEA ARSENAL.. - BZONE

MAMA AISHI KWENYE KONTENA MTOTO ANACHEZEA ARSENAL..

Share This
Mama yake anahisi kuwa mwanae ameambiwa akae nae mbali kwajili ya usalama wa soka lake.
Nyota wa Arsenal Ainsley Maitland-Nile mama yake ametoa ya moyoni na kusema kwamba yeye ni mama tu wa nyumbani asiekuwa na lolote na anaishi kwenye kontena la futi 10.
Jule Nile mwenye umri wa miaka 38  amesema kumekuwa na mtu anapita kati yao na kumpa mwanae maneno yaliyo sio sahihi na kudhihilisha kwamba yeye anaishi kwenye kontena la njano ambapo mda huo huo mwanae anaishi kwenye nyumba ya £700,000 London kaskazini.

“Ni kontena la chuma ambalo alinamadirisha wala kapeti. Hakuna choo wala vitu vya kuogea,” Jule ambae ni mlezi wa watoto aliliambia gazeti la The Sun leo Jumapili.

“Mwanangu Ainsley anaweza kuninunulia mimi nyumba kwa mshahara wake wa wiki 2 au miezi miwili. Mwanangu anachezea Arsenal na mimi ni mama wa nyumbani na sina kitu chochote.”

Maitland Niles yupo kwenye mkataba wa £30,000 kwa wiki pale Arsenal na ameshacheza michezo 21 kwa washika mitutu msimu huu.

“Hakutokuwa na tatizo lolote kama hatakosa pesa zote kesho. Yeye na Cordi ni wanangu na nina wapenda sana nataka wao wajue ilo”


Kwa mujibu wa Maitland Niles aliliambia gazeti la The sun kuwa yeye ajui iyo ishu kama anaishi kwenye kontena na amekuwa akimpa ela kila siku na ataendelea kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment

Pages