Yanga kesho ataingia dimbina akiwa nyumbani kuumana na Stand United ambao waliwalazimisha watani zao sare ya 3-3 huku watani zao wakiomba kusogezewa mchezo wao wa ligi kuu mbele ili kupata mdaa wa kupumzika na kujiandaa kukipiga dhidi ya Al Masry ya Misri huku full back wa kulia kutokea Yanga Juma Abdul akitokea na kuwapa mashabiki zao Moyo kwamba ubingwa wa ligi kuu wanabeba na kimataifa bado wataendelea kulindima.
"Kikubwa ninaomba mashabiki wa Yanga wajitokeze katika mchezo wa kesho, uwepo wao unatupa hamasa ya sisi kupambana uwanjani. Ubingwa unawezekana, hakuna kukata tamaa" alisema Abdul.
Yanga itakuwa ina kibarua dhidi ya Stand United, mechi ambayo kama Yanga itashinda itapunguza pengo la alama kuwa 3 dhidi ya Simba inayoongoza Ligi
No comments:
Post a Comment