ARSENAL WANAANZA KUTAWANYIKA SASA CHINI YA ARSENE WENGER AMEKOSA MASHABIKI,WACHEZAJI NA KLABU. SIO MPAKA 2019 SISI TUNATAKA SASA HIVI. - BZONE

ARSENAL WANAANZA KUTAWANYIKA SASA CHINI YA ARSENE WENGER AMEKOSA MASHABIKI,WACHEZAJI NA KLABU. SIO MPAKA 2019 SISI TUNATAKA SASA HIVI.

Share This
Kila mda ukimfkilia Arsene Wenger unaona kabisa amefikia kiwango cha mwisho, hii timu ya Arsenal inatakiwa itafute njia.

Hakuna Uongozi, hakuna moyo na hakuna mtu muhimu. Sasa wanahaibisha, wanasaliti utamaduni wa Arsenal chini ya uongozi wa Wenger.

Nusu ya timu wamekosa kujiamini na nusu nyingine inaonekana kama hawamtaki Wenger, sio tangia Oktoba 2002 Arsenal walipoteza michezo minne na walionekana wakiwa na kiwango kizuri ni ngumu kujua nini kitafatia kwenye mchezo ujao watashinda au watapoteza.

Arsenal inatawanyika upangiliaji wa Wenger na timu yake bado kabisa hawajaelewana si kimwili wala akili na wanaonekana hawapon teyari kwajili ya kupambana.

Mesut Ozil alitembea kipindi cha kwanza kizima, Henrikh Mkhitaryan alikuwa na udhaifu mkubwa sana kwa leo na Pierre-Emerick Aubameyang alionekana kupoteza umakini kabisa ndani ya uwanja na amini ata yeye mwenyewe ule ujinga aliofanya ndani ya uwanja.

Mashabiki wa Arsenal wanaotoka miji mingine na mataifa mengine ukiachilia wale wa London wamesikika wakisema "We want Wenger Out" wakati wa kipindi cha kwanza huku timu yao ikiwa ishapokea kichapo cha goli 2-0. kulikuwa hakuna mabango yoyote, hakuna ndege yoyote ilio pita juu lakini ilikuwa ni juhudi za kelele kutoka kwa mashabiki ambao wameshachoshwa mpaka sasa na mwenendo wa timu yao.

Sasa hii inatakiwa ifikie mwisho, Wenger akae akijua kashapoteza mashabiki, wachezaji na klabu yake imeshapoteza muelekeo  kwenye kipenga cha mwisho goli kipa wa Arsenal Petr Cech alikuwa akilaumiwa kuwa chanzo cha magoli yote ya Brighton na bila aibu akaenda kwa mashabiki waliosafiri kuja kuipa hamasa timu na akawa rushia jezi yake kwa ishara ya kuomba msamaha ambapo hapo hapo Granit xhaka akitingisha kichwa chake.

Yani walionekana kabisa wamepotea sijui nani hanajua kitachoenda kuwatokea huko mbeleni maana wakumbuke wanaenda kukutana na Ac Milan mpya kwenye michuano ya Europa Alhamisi. 

Ukweli wote tunaujua na tunajifanya kama atuujui tunauweka nyuma tunaitaji mwokozi kusema ukweli na kiukweli Arsenal bado wa sita hebu jaribuni kukumbuka mlivo kuwa mkiwacheka vijana wa Fergie walipokuwa wakishika nafasi ya sita na saba unazani ni nini kilicho  wafanya wao na ni nyinyi muwe nafasi ya sita.

Brighton walikuwa na hasira sana wakiwa na nguvu za kutosha, mashabiki wa kwao na uwanja wao.

Arsenal mpaka sasa wameshaishiwa na mawazo ya kiufundi, wameishiwa nguvu na maisha chini ya wenger na sasa wanachelewa na wakati huku kwetu unaambiwa chelewa chelewa mwana si wako na waswahili wanakwambia ngoja ngoja huumiza matumbo msimu ndo huu unakatika  shauri yenu.

No comments:

Post a Comment

Pages