TATIZO NINI? CHELSEA WAKUBALI MBELE YA WATFORD WALIFANYA IONEKANE KAMA WACHEZAJI WAMECHOSHWA NA ANTONIO CONTE - BZONE

TATIZO NINI? CHELSEA WAKUBALI MBELE YA WATFORD WALIFANYA IONEKANE KAMA WACHEZAJI WAMECHOSHWA NA ANTONIO CONTE

Share This
Antonio Conte ataka ujumbe kutoka bodi ya Chelsea lakini amepata moja wapo kutoka kwa wachezaji.
Chelsea wamekuwa wakifukuza makocha kutokana na kiwango cha timu na kuchechemea kwao inaweza ikamuachia Conte akiwa kwenye hali ngumu na hatari.

Mmiliki wa timu hiyo Roman Abrahomivic aliweza kufukuza makocha nane ndani ya miaka 14 na ilikuwa na hali ilikuwa haipo sawa  ni kwanini Conte aliomba ujumbe kutoka Kwa MASHABIKI kwajili ya kupata ujumbe kutokea bodi.

Lakini licha ya hivo bodi ya Chelsea imekaa kimya licha ya kupata hali ya mshtuko kwenye timu na majanga ya Conte kwa ushahidi huu wachezaji wamechoshwa na Conte.

Watford walibadilisha ubao wa magoli kwa kuwahibisha kwenye dakika za majeruhi ambapo daryl Janmaat, Gerard Deulofeu na Robert Pereyra walishinda magoli matatu ndani ya dakika saba za mwisho na kuishiab 4-1

Niliwaacha mashabiki wa Chelsea wakilalamika "afukuzwe mapema tuu" kwa Conte ambae amekuwa ni shujaa anaetembea kwenye kamba iliokazwa na hali kama hii imekuwa ikiwatokea makocha walio wengi ndani ya Chelsea

Chelsea walikuwa hoi kwakukosa kuoana ndani ya nyoyo zao au hawakuwa na upiganaji wa kuchimba chini zaidi kwajili ya kocha wao ambae anaonekana kutofaidika na kiwango kilichopo ndani ya msimu huu ukitofautisha na msimu uliopita jinsi walivoweza kubeba kombe

walicheza karibia na lisaa wakiwa na watu kumi uwanjani kufuatia Tiemoue Bakayoko kupewa kadi nyekundu na hiyo isiwe sababu kwa jinsi vijana wa  Conte walivoshuka kiwango.

Ni mara ya kwanza Chelsea wanapata mateso ya kupoteza mara kwa mara tangia mwaka 1995. Wanakosa mchanganuo mbele ya macho yetu na hicho ndio kinachomfanyaga Abramovich kupaniki na kufukuza makocha.

Na kama mchezaji mmoja ambae ameleta matatizo ndani ya Chelsea nahisi atakuwa ni Bakayoko.

Usajili wa pauni 40milioni akitokea Monaco amekuwa akiwavunja watu moyo pale alipotolewa, control yake ambayo sio nzuri kwenye mpira uliweza kumtoka na akajikuta akimkanyaga Richarlison ulikuwa ni upumbavu na Refa Mike Dean akuwa na hatua yeyote zaidi ya kumtoa nje. 

Mashabiki wa Chelsea walikuwa wakiliimba jina la Conte na bado wanampenda kwa kile alichofanya msimu uliopita  kwa wengine inaweza ikawa ni kumbukumbu ndogo sana.

JE UNAZANI CONTE ATABAKIA MSIMU UJAO?  

No comments:

Post a Comment

Pages