'HIKI NDICHO NITAKACHO MUULIZA MESSI TUTAKAPO KUTANA' DANNY DRINKWATER - BZONE

'HIKI NDICHO NITAKACHO MUULIZA MESSI TUTAKAPO KUTANA' DANNY DRINKWATER

Share This
Danny Drinkwater ametoa yaliyomoyoni jinsi mipango yake jinsi ilivyo kwa kumuuliza Lionel Messi pale Chelsea itakapo kutana na Barcelona mwezi huu.

Antonio Conte kwa upande wake atakutana na viongozi wa La l;iga kwenye  michuano ya klabu bingwa ulaya kwenye hatua ya mtoano kwente dimba la Stamford Bridge mchezo utakao pigwa Februari 20.

Vilabu hivo viwili vitacheza mchezo wa marudiano kwenye dimba la Nou Camp Machi 14 na wote wanapigania ubingwa wa Ulaya.

Pale alipo ulizwa kuhusiana na Barcelona, Drinwater aliongea wakati wa kufungua kiatu cha Adidas na akasema " ndio na sizani kama nimewahi kucheza kwenye dimba la Nou Camp huko nyuma"

"Nimecheza na Barcelona kwenye mechi za pre seasonmwaka mmoja uliopita lakini Nou Camp itakuwa ni ujuzi mpya naenda kupata na nina hamu ya kucheza pale"

Pale mtu anavokuwaga na shauku ya kukutana na Messi Drinkwater akaongezea "Nilikuwa nikimuangalia kwa mara ya kwanza nilipo cheza naye kwahiyo sijui na sizani nahisi itakua hii ni mara ya pili nitataka nipate jezi yake tuu."

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ametoa ya moyoni kuhusiana muagentina ambaye ni moja kati ya wachezaji bora duniani na akasema mbali na kukutana naye kwenye mchezo wa pre season hana historia ya kukutana na Messi sehemu nyingine na akaelezea hivi "uwezi kusoma kwa kile anachokifanya  ni mwepesi sana kwenye mpira na hanajua kubadilisha mwelekeo" 

"sijawahi kucheza dhidi ya mtu kama yeye nimecheza na watu ambao wanaweza wakabadilisha mwelekeo haraka lakini sio yeye yupo kiwango kingine kabisa"

No comments:

Post a Comment

Pages