SILAHA YA SIRI NYUMA YA WASHAMBULIAJI WA LIVERPOOL NA SIO MO SALAH, SADIO MANE AU MCHEZAJI YEYOTE..... - BZONE

SILAHA YA SIRI NYUMA YA WASHAMBULIAJI WA LIVERPOOL NA SIO MO SALAH, SADIO MANE AU MCHEZAJI YEYOTE.....

Share This
Sahau kuhusu kiwango cha Salah na usambazaji wa Sadio Mane, kuna siri nyuma ya silaha hizi za Liverpool kwenye msimu huu.....Ni  jezi zao zenye rangi ya Chungwa.

Jezi zao za tatu za ugenini almaarufu zinaitwa 'Bold citrus' imedhilisha kuwa na magoli mengi sana majogo hawa wakivaa hii inaweza ikawa ile uchungwa?

Mane aliweza kupata hat trick dhidi ya Porto katikati ya wiki lakini Salah ambae anaefurahia kuvaa langi hiyoo, ameshinda magoli 30 kwenye jumla ya michezo 36 kwa kiwango cha magoli 0.83
sio mbaya kwa winga na akivaa rangi ya chungwa ameshinda magoli tisa kwenye michezo sita.

Wakiwa na rangi ya chungwa wanashinda michezo ya ugenini tuu, baaada ya kuzindua jezi za rangi ya chungwa iliwachukua kusubiri miezi miwili kabla ya kuanza kuzichezea na wakianza nazo kwa kuweka rekodi ya magoli 7-0 wakicheza na Maribor ambapo Salah alishinda mara 2 na vile vile akashinda magoli mawili na West Ham bila kusahau na ile ya Stoke japo alikuwa amekaa kwenye benchi na akaingia dakika 25 za mwisho, tangia Salah ashinde kwenye kila michezo hiyo mitatu  basi imekuwa heri kila pale watakapo vaa jezi hizo.

Mane aliingia kwenye ulingo alipokuwa Ureno dhidi ya Porto na kutangazwa mchezaji bora wa wiki kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya akiwaangusha Cristiano Ronaldo na Iikay Gundogan kupata heshima hiyo.

Washambuliaji hao wawili waliweza kupumzika kwa siku ya jana huku wakifanya mazoezi na klabu yao ilio weka kambi kwenye nji wa Marbella huku Klopp akimkaribisha Nathaniel Clyne kwenye kikosi.

No comments:

Post a Comment

Pages