
Lakini rapa huyo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii siku ya alhamisi alithibitisha kuwa amejiunga na Universal Music.
“By the way I’m Universal Music now” aliandika hivyo Nasty C huku picha ya posti hiyo ikionyesha akiwa amesimama pembeni ya skrini za TV zinazo onyesha alama ya kampuni pamoja na picha yake. Mapema wiki hii rapa huyo alionekana kwenye mkutano na bodi ya wawakilishi wa studio hiyo. Nasty C alijiunga na lebo ya Mabala Noise mwaka 2016, baada ya kukataa dili la Roc Nation ya Jay Z.
Rapa huyo aliishukuru studio ya Mabala Noise kwa msaada wao na aliahidi kuwa lazima ashinde tuzo za Grammy. “Mabala Noise is still and will always be family. Reggie Nkabinde you are going to promise to continue opening doors for our youth and motivating them to aim high, G! P.S. I’m bringing you up on stage when I get my Grammy.”
No comments:
Post a Comment