MANCHESTER UNITED AMESHINDWA KUWAIGA WENZAKE HUKU DAVID DE GEA AKIWASHUJAA ALIWEZA KUWALINDA WENZAKE MZUNGUKO WA KWANZA...!!! - BZONE

MANCHESTER UNITED AMESHINDWA KUWAIGA WENZAKE HUKU DAVID DE GEA AKIWASHUJAA ALIWEZA KUWALINDA WENZAKE MZUNGUKO WA KWANZA...!!!

Share This
Na Bwherever,

Kiukweli Manchester United walikuwa na bahati sana na uthibitisho upo, inabidi wapandishe kiwango chao kama wanataka wasonge hatua ya nane bora.....

Baada ya ushujaa tuliouona kutoka kwenye vilabu vya kingereza kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya, ikawa zamu ya Manchester United ambao walitoka wakiwa flat.

Ligi kuu ya uingereza imegeuka kuwa na mtindo wake wa kipekee msimu huu, Manchester City ambao waliwachapa Basel 4-0, huku Liverpool wakiwagonga nyundo 5-0 Porto na Tottenham ambao waliweza kutokea nyuma kwa 2-0 na kuwa nguvu sawa dhidi ya Juventus.

Chelsea waliweza kuwabana mbavu magwiji Barcelona wakiwa nyumbani lakini United walifanya kazi na wanatakiwa wafanye kazi ya ziada wakirudi nyumbani,bila ya ushujaa wa david De Gea sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine aliefanya uokozi wa hali ya juu kabla ya mapumziko.

Kama ilivyo 0-0  wakiwa ugenini siku zote Sir Alex  Ferguson siku zote anaisomaga "HATARI" akimuacha Mourinho kwa upande wake akiwa na mtihani mkubwa kwenye kichwa chake akujaribu kupata ata goli la ugenini ngoja tuone Machi 13.

Paul Pogba aliwekwa benchi na Mourinho lakini ilibidi amuingize kwenye mapambano kwenye kipindi cha kwanza kuziba pengo la Ander Herera na wengi atukutarajia kama angeingizwa uwanjani lakini Pogba mbali na Mourinho anamuweka nje yeye kama yeye binafsi hayupo kwenye kiwango chake alishindwa kuisaidia timu yake na ameshindwa kutuonesha kwamba yeye ni mchezaji anaetakiwa kutoa amri ya mchezo.

United ambao wanashika nafasi ya pili kwenye ligi walibanwa mbavu na Sevilla ambao wanashikilia nafasi ya tano kwenye La Liga 

Kwa upande wao walikuwa na washambuliaji wenye vipaji pekee kama Alexis Sanchez, Romelu Lukaku, Juan Mata na Pogba ambae alieingia akitokea benchi lakini wenyeji walijitahidi sana kuzuia na kwa haraka na wakimpa wakati mgumu Degea.

Herera alimuweka Sanchez kwenye nafasi tamu sana baada ya dakika 12 lakini mguso wake wa kwanza ulikuwa mzito mguuni kwake na kuwafanya wlinzi wa sevilla kuupata mpira kwa kirahisi.

Mshambuliaji wa Sevilla  Muriel aliwasumbua sana safu ya ulinzi ya United lakini Degea na wenzake waliweza kumzuia asipate goli.

Ilikuwa ni stori ile ile kwenye kipindi cha pili United walilazimishwa kuzuia na huku Sevilla wakimiliki mchezo ndani ya dakika saba za mwisho lukaku aliweka mpira wavuni lakini alikuwa ameunawa na mkono na kufanya kumaliza mchezo bila magoli yoyote,.

Unazani nani atasonga kwenye hatua inayofuata?

No comments:

Post a Comment

Pages