

Kane anaenda kukutana uso kwa uso na na beki wa kitaliano kwenye mji wa Turin kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya kwenye hatua ya 16 bora na kitakua kipimo kigumu sana kwao.

Chiellini mwenye umri wa miaka 33 anaamini kwamba huwezi ukaweka dau kwa mshambuliaji wa kingereza lakini vile vile amewatahadharisha mashabiki wa Spurs watampoteza mchezajin wao hasa Real Madrid wakiingilia kati.
Alisema "Kane kwa sasa amekuwa ni moja kati ya wachezaji wakubwa wanaotazamwa kwa wingi Duniani. Kwa miaka iliopita pamoja na magoli alioshinda amekuwa kwenye kiwangon kizuri sana.

"Messi,Ronaldo, Neymar, Kane amekuwa kwenye kiwango sawa na chao amekuwa ni moja kati ya wachezaji wanajumuishiwa nao na nina uhakika Tottenham watafanya kila linalowezekqana ili aweze kusalia.
No comments:
Post a Comment