HIVI JORGINHO NI NANI? MBONI YA LIVERPOOL INAYOWINDWA KWA UMAKINI... - BZONE

HIVI JORGINHO NI NANI? MBONI YA LIVERPOOL INAYOWINDWA KWA UMAKINI...

Share This

Na Bwherever

Mchezaji wa kiitaliano ambae amecheza kwa moyo wake akiwa na Napoli kama kiungo tokea mwaka 2014 na Liverpool inasemekana wanamuhitaji.....

Jurgen klopp anatafuta nyongeza nyingine Liverpool.
Mbali na kuwa bora kwenye ligi kuu uingereza na kuinusa robo fainali ya klabu bingwa ulaya bado anaangalia mbele kueleka dirisha la usajili pale litakapo funguliwa.

Tukiwa tunaendelea kuona timu ya Liverpool inafanya vizuri hakuna swali lolote  la kuuliza hapa, inasemekana Klopp anatafuta sura mpya Anfield ili kuendelea kuimalisha kikosi chake msimu ujao.

Naby keita atatua akitokea RB Leizipig akiwa anatazamiwa kuwa namba sita wa Klopp, Ripoti zimenasa kwamba Liverpool sasa wameingia kwenye mbio za kumnasa kiungo wa Napoli Jorginho mbali na kwamba watakutana na ushindani mkubwa tokea kwenye vilabu tofauti ulaya, lakini kuna vitu vingine atuvijui juu ya kiungo huyu na nini ataleta pale Anfield.

Atacheza wapi? 

Yeye ni kiungo mkabaji kihalisia kabisa akiwa akiendesha base ya Maurizio kwa mfumo wa 4-3-3 akiwa amecheza michezo 26 msimu huu amekuwa kakiaaa vyema mbele ya beki nne.

Anampangilio gani kwenye uchezaji wake?

Akiwa kama kiungo mkabaji lakini akiwa na miguso yenye utundu na ufundi ndani yake mbali na hiyo ni mwepesi sana pale anapokuwa ndani ya dimba akiwa na rafu zenye akili mbazo zinaweza zikamuumiza kichwa refa kutoa kadi.
amekuwa na pasi 32 muhimu msimu huu amekuwa akipangilia mashambulizi ya kuwasaidia Lorenzo, Mertens, callejon na Hamsik.

Liverpool wapi atakua anafaa? 

Kushindana na Jordan Henderson pale kati kunaweza kukaleta ubora zaidi bila kusahau kukiwa na Emre Can ambae ajui hatma ya maisha yake ndani ya Anfield  ila Jorginho anaweza akaleta chaguo lilo zuri kwa Emre Can na kuamua hatma yake.

Je kuna kitu kingine tunaweza kukijua?

Anapiga penati na amishinda magoli manne ya penati msimu huu.

Je anaweza akaenda Anfield?

Wakala wake anafikilia mteja wake anaweza akaondoka San paolo mbali na Liverpool ambao wameonesha nia lakini kuna timu nyingine zimesha peleka ofa.

Atarudi kuvaa jezi ya Brazili tena au hapo baadae?

ata sielewi...!

Japo alizaliwa kusini mwa mji wa Imbituba uliokuwepo Brazili, Jorginho kwasasa ana miliki passport ya Italia na uraia wa Taifa ilo akiwa na Majina matatu.

No comments:

Post a Comment

Pages