Arsenal walikuwa wabaya. hakuna kuvumila sasa khaa imezidi sasa, Kibaya inamaana ni kitu kisichokuwa na ladha....
Sijisikii kabisa hamua ya kuonja wala kula, kwa timu ambayo imesumbuliwa na Manchester city, najiona kama kipofu, tulikuwa wadhaifu, tusiovutia, tusiokuwa na mipango na ufundi wa kiushindani. Hatuna kiongozi yeyote kama Tony Adams au Patrick Vieira, tumekuwa laini sana na wachezaji hawajui ata kupambana.
Wenger aliangalia hukumu ya kifo huku akisubiria kuchukuliwa kupelekwa kwenye kiti chenye umeme; hasira, mawazo, kutengwa na unyonge ndani yake. Arsenal wamekuwa chini ya kiwango ikiwa kama klabu kubwa kabla ya macho yangu ni mda Arsenal Wenger na Arsenal ikiwa kama kampuni sio timu.
MANENO MAZITOO SIO?
Tupo nafasi ya sita kwenye ligi tukiwa na alama 27 nyuma ya alama kumi kwa mtu anaeshika nafasi ya nne ambayo wanshikilia Tottenham, tumetolewa kwenye kombe la FA yani tumedharilika sana kwenye kombe la ligi na tupo kwenye hatari kubwa ya kutoka kwenye kombe la Europa dhidi ya Ac milan.
Msimu uliopita Wenger alikuwa mbaya kwenye klabu, sasa bora ata msimu ule msimu huu ndio mbaya zaidi na bado anaendelea anaipeleka timu kwenye mapinduzi yalio mabaya na bado hataki tu kutoka...
Gwiji wa Arsenal Ian Wright aliiweka hii vizuri jana Jumapili na alisema ' kumuangalia Wenger kwa sasa ni kama kuwa shahidi kwenye pambano la Muhamad Ali dhidi ya Larry Holmes au kumuangalia mshambuliaji wa Barzil Ronaldo anavokuwa kibonge, tatizo la Arsenal Wenger kwamba hakuna mtu ambae yupo teyari kumrushia taulo pale anapokatiza kwenye mitaa'

Jumapili ilikuwan ni siku ya kuaibika kwa Wenger na Arsenal yake haiwezi kuendelea hivi kwajili yake mwenyewe na usalama wa klabu na kwa usalama wa mashabiki Mungu wangu we nenda tuu tumechoka.
No comments:
Post a Comment