SANCHEZ KURUDISHA HESHIMA YA JEZI NAMBA 7? - BZONE

SANCHEZ KURUDISHA HESHIMA YA JEZI NAMBA 7?

Share This
By Martin
Juzi zilipatikana dakika 72 za kwanza za Alexis Sanchez.
Dakika 72 ambazo zilimwezesha awe mchezaji bora wa mechi ya jana ya
FA CUP dhidi ya Yeovil Town.
Hii inatoa tafasri moja, ulikuwa mwanzo mzuri wa Sanchez ikizingatia
kila jicho lilikuwa linamtazama yeye kila aliposhika mpira.
Lakini hofu aliishusha chini, akawa hana presha kubwa juu ya mechi
yake ya kwanza akiwa na uzi wa Manchester United.
Miaka 3 amekuwa nchini England, akicheza Arsenal. Hakuwa mgeni na soka
la Englnad hali ambayo ilimfanya yeye asiwe na wakati mgumu katika
mchezo wake wa kwanza.
Juzi Manchester United walicheza mfumo gani ?
Kwenye karatasi Manchester United walianza na mfumo wa 4-3-3, lakini
kwenye uwanja ilikuwa tofauti, kwani walikuwa wanacheza mfumo wa
4-3-2-1. Mabeki wa kati wakiwa Rojo, Lindelof. Beki wa pembeni kulia
alikuw a Darmian na beki wa pembeni kushoto alikuwa Luke Shaw.
Wakati viungo watatu wa kati walikuwa Carrick, Scott McTommy na Ander Herrera.
Mbele yao alicheza Mata ambapo eneo la kushoto mbele alicheza Sanchez
ambaye alikuwa anatokea pembeni kushoto akiingia katikati , huku
Rashford akiwa mchezaji wa mwisho.
Yeovil Town walicheza mfumo wa 4-4-2 , ambapo uliwawezesha kipindi cha
kwanza wacheze kwa kuelewana na kujilinda vizuri.
Njia pekee ambayo walikuwa wanaitumia kujilinda ni kuhakikisha
hawatengenezi uwazi eneo la nyuma ndiyo maana kipindi cha kwanza
ilikuwa ngumu kwa Manchester United kutengeneza nafasi nyingi za wazi
kwa sababu hakukuwepo na uwazi sehemu ya nyuma ya Yeovil Town.
Pia wachezaji wa Yeovil Town walikuwa wana “mark” kila mchezaji wa
Manchester United alipokuwa anapata mpira.
Hivo wachezaji wa Manchester United hawakuwa huru kutengeneza nafasi
kila wanapopata mpira kwa sababu wachezaji wa Yeovil Town waliwakaba
“man to man”.
Yeovil Town walikuwa wanashambulia kwa kutumia mipira ya moja kwa moja
“direct football” ingawa hawakuweza kutumia vizuri mashambulizi yao
kwa sababu ya kukosa ukomavu.
Kuna wakati Yeovil Town waliwalazimisha Manchester United kufanya
madhambi karibu na eneo lao , kwa kipindi cha kwanza pekee Manchester
United walifanya madhambi mara 7 dhidi ya mara 3 ya Yeovil Town,
lakini Yeovil Town hawakuwa na nidhamu nzuri ya matumizi mazuri ya
mipira ya adhabu waliyokuwa wanaipiga.
Manchester United walibadilisha mfumo kipindi cha pili.
Baada ya Lukaku kuingia nafasi ya Mata, Manchester United walicheza
4-3-3 halisi ambapo katikati walibaki Carrick, Scott na Herrera na
mbele wakabaki Sanchez kushoto, Rashford kulia na katikati akasimama
Lukaku.
Kipindi hiki cha pili Yeovil Town waliachia uwazi katika maeneo mengi
ya uwanja hasa hasa nyuma ndipo hapo Manchester United walitumia
vizuri nafasi hiyo ambapo kipindi cha kwanza hakukuwepo na uwazi
katika maeneo ya nyuma ya Yeovil Town.
Baada ya Sanchez kuondoka na kuingia Lingard Manchester United
walirudi tena kwenye mfumo wa 4-3-2-1, ambapo Lingard alikuwa anatokea
katikati na kucheza nyuma ya Lukaku aliyesimama kama mshambuliaji wa
mwisho wakati Rashford akicheza pembeni kushoto.
Je Luke Show anatakiwa kuongezewa mkataba ?
Amekaaa muda mwingi akiwa majeruhi, ndiye mchezaji pekee kwenye kikosi
cha Manchester United ambaye ni namba tatu halisi.
Mkataba wake unaisha katika majira ya joto, lakini kadri muda
unavyozidi kwenda anaonesha kuwa anastahili mkataba mpya kulingana na
kiwango chake anachokionesha baada ya kuaminiwa.
Sanchez atarudisha heshima ya jezi namba saba?
Bryan Robson ambaye alikuwa anajulikana kama “Captain Marvel”) alikuwa
na kiwango kizuri na kikubwa chenye mafanikio makubwa akiwa na jezi
namba 7, ambapo baadaye Eric Cantona alifanikiwa kupata mafanikio
makubwa na jezi hiyo kama ilivyokuwa kwa David Beckham na Cristiano
Ronaldo.
Baada ya Cristiano Ronaldo kuihama timu hii mwaka 2009 hakuna mtu
aliyefanya vizuri na jezi hii.
Walivaa kina Michael Owen, Di Maria, Valencia, Depay lakini hakuna
aliyefanya vizuri na jezi hii. Valencia alivaa mwaka mmoja
akairudisha.
Ni jezi nzito katika klabu ya Manchester United, leo hii Sanchez
amepewa aibebe mgongoni, mafanikio aliyoyapata na Arsenal, kwa
kiwango kile alichokionesha katika nchi ya England kwa miaka 3 kunampa
nafasi ya kufanya vizuri na jezi hii ingawa umri unamnyima nafasi ya
kufanya makubwa zaidi

No comments:

Post a Comment

Pages