Chelsea wataendelea na mazungumzo na Roma kuhusu Edin Dzeko leo Jumatatu.
'kama unaona kikosi chetu hakina washambuliaji watatu, wanne au watano tuna washambuliaji wawili tu ambao ni Alvaro Morata na Batshuayi,' alisema Conte.
'klabu itaenda kufanya maamuzi mazuri kwa kuongeza wachezaji au kuendelea na washambuliaji wawili. Nitakuwa na furaha kwa maamuzi yote mawili'
'Inabidi tuangalie nini kitatokea kwenye soko.'
Batshuayi hana magoli 10 msimu huu na akiwa ameanza michezo 19 lakini Conte anaonekana anataka chaguo jengine akiwa na pauni milioni 25 kwajili ya kumpata Edin Dzeko.
'Nina fanya kazi kila siku na leo nina furaha sana hapa,' alisema Batshuayi 'sijui juu ya maisha yangu mbeleni yatakuwa vipi, ni bora muongee na Conte.'
Conte alinukuliwa mapema ya wiki hii kwamba ata mruhusu Batshuayi kutumia msimu wake wote sehemu nyingine kama masharti yake yatakuwa sawa.
No comments:
Post a Comment