"Nafasi ya Okwi kucheza ilitakiwa ichukuliwe na Mavugo" MASOUD DJUMA - BZONE

"Nafasi ya Okwi kucheza ilitakiwa ichukuliwe na Mavugo" MASOUD DJUMA

Share This
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa ushindi ambao timu yake iliyoupata jana Alhamisi katika mchezo dhidi ya Singida United ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya wachezaji wake huku akimtolea ‘povu’ straika wale Laudit Mavugo.

Simba ilipata ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya wababe hao wa Singida ambapo mabao yake yalifungwa na Shiza Kichuya, Asante Kwasi na Emmanuel Okwi aliyefunga mawili.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Djuma alisema nafasi ya Okwi kucheza ilitakiwa ichukuliwe na Mavugo lakini kwa kuwa Mavugo hakuonyesha kiwango kizuri mazoezini ilimbidi afanye mabadiliko hayo.

“Okwi amefanya mazoezi na sisi siku mbili tu kama mnavyojua hakuwepo kambini, nilipanga kumtumia Mavugo lakini nimemwambia kuwa hakuonyesha uwezo mzuri, ndiyo maana nikaamua kumpa nafasi Okwi na kweli ameitumia vizuri.

“Nimeshamueleza Mavugo kuwa yeye ni ndugu yangu lakini katika hili suala la kazi anatakiwa kuonyesha uwezo na kufanya kweli, siwezi kumpa nafasi kama haonyeshi uwezo,” alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages