MANCHESTER CITY WAJIPA MATUMAINI KWA KUPATA SAHIHI YA BEKI KUTOKEA ATHLETIC BILBAO - BZONE

MANCHESTER CITY WAJIPA MATUMAINI KWA KUPATA SAHIHI YA BEKI KUTOKEA ATHLETIC BILBAO

Share This
Kocha wa city Pep Guardiola ameshawishwi sana na mchezaji mwenye umri wa miaka 23 kwa mda sasa na amekubali kukutana nae.

Dili la Mfaransa ambae anacheza kama beki wa kati bado alijawa wazi lakini mazungumzo teyari yameshaanza na yanaweza kukamilika kabla ya dirisha la usajili kufungwa wiki ijayo.

Rekodi kubwa waliofanya city kwenye usajili ilikuwa tokea mwaka 2015 pale walipo msajili Kevin De Bruyne kwa ada ya pauni milioni 55 akitokea Wolfsburg na kwasasa ameongeza mkataba ambao utakao muweka Etihad mpaka mwaka 2023.


Aymeric Laporte amekuwa akiongelewa kati ya mabeki wadogo wenye thaman kubwa sana kwenye La liga lakini kwasasa ameweza kucheza timu ya vijana Ufaransa.

Alijiunga na Bilbao akiwa na miaka 16 na ameshinda magoli 10 kwenye michezo 222 kwenye klabu ya Basque na vile vile akiwakilisha ufaransa mara 19 kwenye timu ya chini ya miaka 21.

pale atakapo wasili atamfanya Guardiola kuwa na beki mwenye thamani ya nyongeza, mbali ya kuwa na chaguo lake la kwanza akiwa na John Stones na Nicolas Otamendi huku Vincent akionekana kutokuwa tena tegemeo la kuaminika huku Guardiola akisema akiwa hana imani na beki wake Eliaquim Mangala kutokuwa na hali ya kutojiamini.

Usajili mkubwa walioufanya Manchester City mpaka sasa.
£55mKevin de BruyneWolfsburg2015
£52mBenjamin MendyMonaco2017
£47.5mJohn StonesEverton2016
£45mKyle WalkerTottenham2017
£44mRaheem SterlingLiverpool2015
City bado wanaonekana kutokata tamaa kumnyemelea beki wa West Brom Jonny Evans lakini mpaka pale Mfaransa Mangala atakapo ondoka wiki ijayo .

No comments:

Post a Comment

Pages