IKUFIKIE HII, KAMUSOKO RASMI MAZOEZINI, AANZA MAZOEZI MEPESI - BZONE

IKUFIKIE HII, KAMUSOKO RASMI MAZOEZINI, AANZA MAZOEZI MEPESI

Share This
Yanga imeendelea kujifua leo huku kiungo wake, Thabani Kamusoko akiendelea na mazoezi binafsi.

Mazoezi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara yamefanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kamusoko alikuwa akiendelea na mazoezi binafsi ya kujifua pembeni ikiwa ni dalili njema kwamba atarejea hivi karibuni.

Kiungo huyo raia wa Zimbabwe amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu sasa huku Yanga ikiendelea kupambana.

No comments:

Post a Comment

Pages