FERNANDO FELICEVICH NI NANI? KUTANA NA MTU ALIEKUWA NYUMA YA DILI LA ALEXIS SANCHEZ. - BZONE

FERNANDO FELICEVICH NI NANI? KUTANA NA MTU ALIEKUWA NYUMA YA DILI LA ALEXIS SANCHEZ.

Share This
Alexis Sanchez anakaribia kutua Manchester lakini anaweza akajiunga na ipi city au United?

Ilionekana kwamba angeweza kutua Etihad moja kwa moja mwezi huu au dirisha kubwa lijalo na mkataba wake ukiwa unakaribia kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Lakini United wapo kwenye nafasi kubwa sana ya kuweza kumnyakua mchile huyo ambapo utakua ni uhamisho wa kushangaza kwa Jose Mourinho.

Wakala wake Fernando Felicevich ni moyo juu ya uhamisho huu na inasemekana anaweza akatia mfukoni pauni milioni 5 mfukoni kwenye dili hili.

Lakini wakala wa nyota huyu wa Arsenal ni nani?

HISTORIA

Felicevich ambae amezaliwa Argentina almaarufu anajulikana kama 'Mfalme wa soka la America Kusini'
Alikuwa mchezaji wa rugby kipindi cha ujana wake na alikuwa anafanya kazi ya kufanya matangazo Chile baada ya akaenda kusoma Paris.
Aliingia kwenye soka akiwa na miaka 33 na baadaye akawa wakala.

THAMANI YAKE IPOJE?

Mwaka 2017 aliweza pata thamani ya pauni milioni 18 na ikamfanya kushika namba sita kwenye Forbes kwenye orodha ya mawakala wakubwa.

NANI YUPO KWENYE VITABU VYAKE?

Felucevich ni wakala wa wachezaji wanaotokea America kusini. Moja ya wachezaji hao pamoja na mchezaji kutokea Bayern Munich Arturo Vidal. 
Vilevile alijihusisha na Gary Medel kwenda Cardiff.

ALIKUTANA VIPI NA SANCHEZ...!

Alikutana na Sanchez pale alipokuwa mdogo kwenye vitabu vya chile upande wa Cobreloa 
Alikuja kuwa wakala wake baada ya kuongea na mama yake Sanchez na kumsaidia kumpeleka Udinese 2006.

Felicevich alikuwa ni kiungo mkubwa sana katika uhamisho wa Barcelona na Arsenal na alikuwa akimsaidia kulinda uhamisho huo uweze kufanyika na kumuwezesha kutua Emirates.

No comments:

Post a Comment

Pages