Dortmund wamethibitisha habari hizi kupitia ukurasa wao wa twitter leo jumatano kabla ya picha zake kusambaa, Aubameyang amekuwa mchezaji wa historia anayelipwa vizuri kwa dili la mkataba wa miaka mitatu na nusu akiwa anapokea mshahara wenye thamani ya pauni 180,000 kwa wiki.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 amekuwa ni moja kati ya uhamisho wa mingi inayoendelea hapa kati na tunaweza tukamuona Olivier Giroud akiwaacha washika mitutu akiwa anatazamiwa akielekea Chelsea na huku Michy Batshuayi akitoka Stamford Bridge ili kuziba pengo la Aubameyang
No comments:
Post a Comment