Luiz Felipe Scolari asema Nicolas Anelka alimfanya afukuzwe Chelsea kwa kukataa kucheza Winga. - BZONE

Luiz Felipe Scolari asema Nicolas Anelka alimfanya afukuzwe Chelsea kwa kukataa kucheza Winga.

Share This
SPORTS: Kocha wa zamani wa Chelsea Luiz Felipe Scolari alisema Nicolas Anelka alifanya yeye afukuzwe Stamford Bridge kwa kutaa kucheza winga.

Mbrazil huyo alipigwa panga na the Blues Februari 2009 baada ya mwaka. Lakini Scolari licha ya kusemwa atumii kingereza kuongea na wachezaji wakee ili aleweke aliweza kupotezea hayo maneno.  Scolari alikuwa na malalamiko makubwa juu ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Liverpool.

Pale Didier Drogba aliporudi kutoka majeruhi Scolari alisema alikutana na washambuliaji wake wote na kumwambia mmoja inabidi acheze winga na hapo vitu ndipo vilipoanza kwenda kombo.

“Nilimweka Anelka acheze mbele. Tisa. Akiwa mfungaju bora ligi kuu,” Scolari aliwaambia ESPN Brazili.

“Wachezaji wakarudi, nikaweka kikao  na kwenye kikao nikasema: ‘angalia sasa wachezaji wote wamerudi  Drogba karudi baada ya miezi miwili, tutajaribu kuifanyia kazi hii hali ya washambuliaji wetu wawili ya wote kucheza sehemu moja itabidi mmoja acheze katikati mwingine ahame upande.’

“Alafu Anelka mfungaji bora wa ligi, alisema. ‘ sitocheza winga mimi!’ Ndio hivi ndivo alivosema. Na mimi nikasema “uchezi winga, mmoja lazima akacheze kushoto nimemaliza, sitokaa hapa kubishana na nyinyi hapa.’



“Niliondoka pale na timu yetu ikaishia nafasi ya tatu kwenye ligi nyuma  ya alama tatu au nne tofauti na waongozaji wa ligi tukafuzu kwenda atua ya 16 bora na robo fainali ya klabu bingwa ulaya. Lakini kulikuwa na haya mazingira mabaya.

“Sijui kama ningeendelea nini kingetokea lakini niliingiliwa ndomana nikakasirika.”
 “Wote walisema . Oh kwasababu ukuongea kingereza vizuri, ndio sikujua ndomana sikuongea vizuri lakini ninajua ninaelewa vizuri.”

No comments:

Post a Comment

Pages