Kocha wa Everton Sam Allardyce anajiandaa kutoa ofa kwa Arsenal ili kumnyakua Theo Walcot na kuwawekea mtego wa kumchukua Steven N'zonzi... - BZONE

Kocha wa Everton Sam Allardyce anajiandaa kutoa ofa kwa Arsenal ili kumnyakua Theo Walcot na kuwawekea mtego wa kumchukua Steven N'zonzi...

Share This
SPORTS: Sam Allardyce anajiandaa kuweka mezani ofa ya kuchukua Theo Walcot.

Na kocha  huyo mpya wa Everton hana matumaini makubwa ya kuweza kutungua ndege wawili kwa jiwe moja kwenye mbio za kumnyakua Theo  Walcot na Steven N'zonzi Januari.

Walcot ambae amebakiza miezi 18 ili mkataba wake wa pauni 140,000 kwa wiki kuweza kukatika. Akiwa ajafanikiwa kuanza mchezo ata mmoja wa ligi msimuu huu.

Allardyce ambae atapewa fungu mwezi ujao ili kuweza kutengeneza kikosi chake  akiwa kama kocha wa kikosi hicho ameweza kusema nia yake kwa mshambuliaji wa Arsenal Walcot kumvuta ndani Goodison Park.

Ofa ya Walcot ambae mwenye umri wa miaka 28 inaweza ikawa tiba kwa Everton ambayo wamekuwa na uhaba wa magoli tangia kuondoka kwa Romelu Lukaku ambae alisajiliwa na Manchester United msimu uliopita.

Na vile vile Allardyce anaonekana akiwa na ujasiri wa kumsajili na N'zonzi. Everton wanamatumaini makubwa ya kumchukua N'zonzi ata kwa  mkopo kwa msimu mzima.

Mchezaji huyo wa zamani wa Blackburn na Stoke ambae Allardyce alimsajili pale alipokuwepo kwenye dimba Ewood Park yupo huru tangia apishane na kocha wake Eduardo Berizzo.

West Ham wanamatumaini pia ya kuweza nao pia kuzima dili ilo la Everton la kumvuta mfaransa huyoo na kuanza mazungumzoo tangia wiki ilio pita.

No comments:

Post a Comment

Pages