TURITARAJIA TUTAITIMISHA MZUNGUKO WA KWANZA KWA KUONGOZA LIGI LAKINI MAMBO YAMEKUWA KINYUME - BZONE

TURITARAJIA TUTAITIMISHA MZUNGUKO WA KWANZA KWA KUONGOZA LIGI LAKINI MAMBO YAMEKUWA KINYUME

Share This
SPORTS: Azam FC imeshindwa kuishusha Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja na Mtibwa Sugar usiku huu uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Matarajio ya mashabiki wa Azam FC yalikuwa ni kuhitimisha mzunguko wa 11 wa VPL kwa kushika usukani baada ya Simba kutoka sare ya 1-1 na Lipuli FC jana, lakini mambo yamekuwa ni kinyume na matarajio hayo.
Kwenye mchezo huo, bao la Azam FC limefungwa na Enock Atta Agyei kwa kichwa baada ya kuruka juu zaidi ya beki wa Mtibwa Sugar ndani ya sita na kumalizia kros iliyochongwa na Mbaraka Yusuph kutoka upande wa kushoto.
Mtibwa Sugar waliopoteza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa Ally Makarani, Stamil Mbonde, na Mohamed Issa, walifuta makosa kwa bao safi la kusawazisha kwa ‘free-kick’ iliyochongwa kwa ufundi na Kelvin Sabato Kongwe dakika chache baada ya kuingia dimbani baada ya kuanzia kwenye benchi.
Kwa matokeo hayo, Simba wanaendelea kuongoza kwa pointi zao 23 sawa na Azam FC katika nafasi ya pili, lakini Simba ina tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku nafasi ya tatu ikishikwa na mabingwa watetezi Yanga wenye alama 21.

No comments:

Post a Comment

Pages