“EBU SAHAU” MANCHESTER UNITED WANAMUWINDA ANTONIE GRIEZMANN ATOA YA MOYONI KAMWE ATOENDA ARSENAL. - BZONE

“EBU SAHAU” MANCHESTER UNITED WANAMUWINDA ANTONIE GRIEZMANN ATOA YA MOYONI KAMWE ATOENDA ARSENAL.

Share This
SPORTS: Antonie Griezman ameweza kusema yake ya moyoni kwamba atokuja kuacha wino wake Arsenal baada ya jinsi walivyomfanyia nyuma ya 2013.

Mchezaji huyo wa kimataifa akitokea Ufaransa alitaarifiwa na Arsene wenger kuwa hana nia naye kupitia skauti wa Arsenal Giles Grimandi ambapo alikuwa bado yupo Real Sociedad. Mchezaji huyo wa Atletico Madrid na taifa la Ufaransa aliweza kumwambia wakala wake kama atokuja kwenda kwa washika bunduki.

Kupitia autobiography yake aliandika na kusema “2013 nilisubiria, nilisubiria na nikaendelea kusubiria, pale palipokuwa hakuna habari Eric aliweza kumuita Grimandi na ambae alisema  kocha bado hana nia na mimi kwahiyo endelea kusubiria.”

“Mwishoni baada ya masaa machache kabla ya dirisha kufungwa akatutaarifu kwamba Arsenal hawatofanya uhamisho. Sipendeleagi kuambiwa kitu alafu mwishoni kisitokee.”

“Pale Eric aliponiambia baadae kwamba klabu iyo kutokea london wanania na mimi bado nikamuambia ‘sahau kuhusu iyo, baada ya kutusubirisha sana.”

Griezman ambae ambae aliweka sahihi yake Atletico Madrid amekuwa na nguvu ya kuhusushwa kunyatiwa na Manchester United miezi michache iliopita baada ya kukosa kumsajili  dirisha kubwa la usajili.

No comments:

Post a Comment

Pages