KUMBE HII BADO IPO...!!!! TULISHASAHAU ETI NAO WAMEPEWA ALAMA ZA MEZANI. - BZONE

KUMBE HII BADO IPO...!!!! TULISHASAHAU ETI NAO WAMEPEWA ALAMA ZA MEZANI.

Share This
TFF TANZANIA
SPORTS: Timu ya JKT Mlale inayoshiriki Ligi daraja la kwanza imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya KMC kumchezesha nahodha wake, Stephano Mwasika katika mechi iliyofanyika Oktoba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex wakati akiwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi maarufu (kamati ya saa 72) na kutangazwa na Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi katika mkutano na wanahabari uliokuwa mbashara kupitia Azam Sports 2.
Wambura amesema Mwasika alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko mpinzani wake kwenye mechi namba 15 kati ya KMC na Mbeya Kwanza iliyochezwa Oktoba 5, 2017 katika Uwanja wa Azam Complex.
Adhabu nyingine zilizotolewa na bodi hiyo kwa vilabu vya ligi daraja la kwanza ni kama ifuatavyo:-
Klabu ya Mvuvumwa imepigwa faini ya 100,000 kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi dhidi ya African Lyon ikiwa na maofisa pungufu kinyume cha kanuni.
Nayo Klabu ya JKT Mlale imepigwa faini ya shilingi 200,000 kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo.
Mtunza vifaa wa Timu ya JKT Mlale, Noel Murish amesimamishwa hadi suala lake la kuwamwagia maji mashabiki wa polisi Tanzania litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Noel alifanya kitendo hicho katika mechi hiyo iliyochezwa Novemba 4, 2017 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Klabu ya Coastal Union imepewa onyo kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi kikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na kanuni. Timu hiyo ilifanya hivyo katika mechi dhidi ya JKT Mlale iliyofanyika Novemba 12, 2017 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Klabu ya Toto Africans imepewa onyo kali kutokana na timu yake kuchelewa kikao cha maandalizi (pre match meeting) katika mechi dhidi ya Biashara United Mara iliyofanyika Novemba 5, 2017 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Meneja wa Toto Africans, Yusufu Jumaa amefungiwa miezi miwili na kupigwa faini ya shilingi 200,000 baada ya kuondolewa na mwamuzi kwenye benchi la ufundi kwa kupinga maamuzi yake na kumshambulia kwa maneno.
Naye afisa habari wa Toto Africans, Cuthbert Japhet amesimamishwa hadi suala lake la kummwagia maji mwamuzi na kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali wakati wa mapumziko katika mechi hiyo litakaposilikizwa na kamati ya nidhamu ya TFF.
Adhabu nyingine zimekwenda kwa waamuzi ambapo waamuzi wasaidizi Jumanne Njige wa Mwanza na Bam Bilasho wa Dodoma wamepewa onyo kali kwa kuchezesha chini ya kiwango mechi ya kundi C kati ya Transit Camp na Rhino Rangers iliyofanyika Novemba 11, 2017 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Pages