Magoli ya Rudiger na Willian yalikuwa yanatosha kuwazima Everton katika dimba la Stamford Bridge na kufanya kuendelea hatua ya nane bora au robo fainali kwenye kombe la Carabao.
Antonio Conte alifanya mabadiliko mara baada ya ushindi dhidi ya Watford Jumapili akimpa Ampadu ambae alicheza kama kiungo wa kati, huku ikitazamiwa ni mchezo wake wa pili huku kennedy akianza kucheza beki mshambuliaji wa kushoto huku Musonda akitumika kama beki wa kushoto.
Na kuongea baada ya mechi, kocha wa kiitaliano alisema vijana hao walicheza mchezo mzuri. Perfomance yao ilikuwa ni nzuri sana hasa kipindi cha kwanza walipotengeneza nafasi za kushinda. Alisema Conte 'kipindi cha pili tuliangaika lakini kidogo sio kawaida hasa unapocheza na timu kama Everton'
'Everton ni timu nzuri na hasa wamebadilisha kocha na sio kawaida yao kuwa kwenye hali kama hiyoo wachezaji wamejaribu kubadilisha na kutupa kitu zaidi, huu mchezo ulikuwa ni hatari sana kwetu sisi'
'Lakini nina furaha sana, usiku wa leo nimeona vitu tofauti sana, wachezaji wadogo jinsi walivoonesha viwango vyao. Charly Musonda, Kenedy na Ampadu wanamiaka 17 tu lakini wamecheza vizuri sana.
No comments:
Post a Comment